Maonyesho ya 139 ya Canton yavutia wanunuzi wa kigeni 245,000 katika vipindi vyake viwili vya kwanza

(Tovuti ya Gazeti la Umma) April 28, 2026

Mnunuzi (kulia) akitazama vitu vinavyooneshwa kwenye Maonyesho ya 139 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China (Maonyesho ya biashara ya Canton), huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Aprili 23, 2026. (Xinhua/Deng Hua)

Mnunuzi (kulia) akitazama vitu vinavyooneshwa kwenye Maonyesho ya 139 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China (Maonyesho ya biashara ya Canton), huko Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Aprili 23, 2026. (Xinhua/Deng Hua)

GUANGZHOU - Maonyesho ya 139 ya Uagizaji na Uuzaji Bidhaa Nje ya China (Maonesho ya Biashara ya Canton) yaliyofanyika katika vipindi vyake viwili vya kwanza yamevutia wanunuzi 245,000 kutoka nchi na maeneo 219 hadi kufikia jana Jumatatu alasiri, ikiwa ni ongezeko la asilimia 2.2 kuliko vipindi kama hivyo vya maonyesho yaliyopita, Kituo cha Biashara ya Nje cha China kimesema.

Kimefafanua kwamba, jumla ya mashirika 140 ya viwanda na biashara ya ng'ambo yameshiriki kwenye maonyesho hayo. Kampuni na viwanda vinavyongoza kwenye sekta vipatavyo 344 kutoka Marekani, Mexico, Uingereza, Ujerumani, na Japan pia vimeshiriki kwenye maonesho hayo, na kufikia ongezeko la asilimia 4.9 kuliko kipindi kama hicho cha maonyesho yaliyopita.

Kituo hicho kisema kuwa, Maonyesho hayo ya mwaka huu yanafanyika kwa vipindi vitatu nje ya mtandao katika Mji wa Guangzhou, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, na yamepangwa kuendelea hadi Mei 5.

Maonesho hayo ya kipindi cha pili yalifanyika kuanzia Aprili 23 hadi 27, ambayo yaliwekwa mkazo katika kuonesha bidhaa za sifa bora zinazochangia "maisha raha nyumbani," ikiwa ni pamoja na raslimali za ujenzi, samani, vifaa na vyombo vya matumizi nyumbani, zawadi na mapambo. Na maoensho hayo ya kipindi chake cha tatu yanapangwa kufanyika kuanzia Mei 1 hadi 5, ambapo bidhaa nyingi zaidi zitakazooneshwa ni kama vile midoli, vitu vinavyotumiwa na mama wazazi na watoto wachanga, nguo na vitu vya vitambaa vya matumizi nyumbani, vitu vya matumizi ya ofisini au masomo darasani , pamoja na bidhaa za afya na burudani.

Maonyesho hayo ya biashara yaliyoanzishwa rasmi mwaka 1957, yanafanyika mara mbili kila mwaka katika Mji wa Guangzhou. Ni maonyesho yanayofanyika kwa muda mrefu zaidi ya shughuli za biashara ya kimataifa nchini China, na yamesifiwa kuwa kipimo cha biashara ya nje ya China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha