Lugha Nyingine
Xi Jinping aongoza mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya CPC kuhusu hali na kazi ya uchumi
BEIJING - Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imefanya mkutano jana Jumanne kwa kuchambua na kujadili hali ya hivi sasa ya uchumi na kazi ya uchumi, ambapo Xi Jinping, Rais wa China ambaye pia ni katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC, aliongoza mkutano huo.
Mkutano huo umeeleza kwamba uchumi wa China umekua na mwanzo mzuri mwaka huu, huku viashiria muhimu vikizidi matarajio, hali ambayo inaonesha uhimilivu na nguvu zake bora.
Hata hivyo, mkutano huo umesema kwamba, uchumi bado unakabiliwa na taabu na changamoto, na msingi wa ufufukaji endelevu wa uchumi wa nchi unahitaji kuimarishwa zaidi. Mkutano huo umetoa wito wa kufanya juhudi kubwa zaidi na kuchukua hatua zenye ufanisi halisi zaidi ili kuhimiza kazi ya uchumi.
Mkutano huo umesema kwamba juhudi zinapaswa kufanywa ili kufikia hali ya kujitegemea na kuwa na nguvu katika sekta ya sayansi na teknolojia, na kujenga minyororo ya viwanda inayojiamulia na inayoweza kudhibitiwa, na pia inayoweza kukabiliana na hatari.
Mkutano huo umesema China inapaswa kutekeleza sera ya bajeti ya kuweza kuhimiza juhudi zaidi, na kutumia sera ya mambo ya fedha yenye unyumbufu wa kufaa kwa kulenga mambo halisi na kwa njia yenye ufanisi, kuendelea kupanua mahitaji ya ndani na kuboresha kazi ya utoaji wa bidhaa.
Mkutano huo umetoa wito wa kufanya juhudi za kuimarisha uchumi wa ndani na kuboresha mzunguko wa uchumi wa ndani na wa kimataifa ili kupata mwanzo mzuri wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano (2026-2030).
Mkutano huo umesisitiza kwamba China inapaswa kutumia vya kutosha sera za jumla, kuboresha miundo ya matumizi ya kibajeti, na kuifanya sera ya mambo ya fedha kuwa ya kutupia macho mbele yenye unyumbufu na kulenga mambo halisi.
Mkutano huo umetoa wito wa kufanya juhudi zaidi za kutafuta na kuongeza mahitaji ya ndani, na kuchukua hatua za kupanua utoaji wa bidhaa zenye sifa bora na huduma bora ili kuhimiza matumizi kupandishwa ngazi.
Kwa mujibu wa mkutano huo, China itatekeleza kwa pande zote mpango wa "AI plus", kuendeleza aina mpya za uchumi wa AI, na kukamilisha usimamizi wa AI.
Mkutano huo umehimiza juhudi za kukabiliana na utaratibu mishtuko na changamoto kutoka nje, kuongeza usalama wa nishati na maliasili ili kuwa na hali ya uhakika wa maendeleo ya sifa bora kwa kukabiliana na hali za kutokuwa na uhakika.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



