Lugha Nyingine
Roboti ya muundo wa binadamu yaipita rekodi ya mbio za nusu marathon duniani ya binadamu mjini Beijing
BEIJING - Roboti ya muundo wa binadamu iliyopewa jina la "Flash" kutoka kampuni ya Maendeleo ya Teknolojia Janja ya Shenzhen Honor imeshinda katika mashindano ya mbio za nusu marathon za Beijing E-Town mwaka 2026 kwa kukimbia kwa muda wa dakika 50 na sekunde 26 katika kipengele cha kukimbia kwa kujitegemea yenyewe jana Jumapili, ikiipita rekodi duniani ya binadamu ya kukimbia kwa muda wa dakika 57 na sekunde 20.
Rekodi ya mbio za nusu marathon duniani kwa wanaume iliwekwa na mkimbiaji nyota wa Uganda Jacob Kiplimo katika mashindano ya mbio za nusu marathon za Lisbon nchini Ureno mwezi uliopita.
Katika mashindano ya kwanza ya mbio hizo za nusu marathon za E-Town mwaka 2025, Tiangong Ultra ilipata ushindi kwa kukimbia kwa muda wa saa mbili, dakika 40, na sekunde 42, na ni timu sita tu kati ya 20 zilizoshindana zilizofanikiwa kumaliza mbio hizo za urefu wa kilomita 21.0975 na kuweka rekodi ya kihistoria.
Katika mashindano hayo ya pili ya jana Jumapili, roboti zenye muundo wa binadamu zimepiga hatua ya aina yake na kuonyesha mafanikio mapya ya kiteknolojia kuwa ya haraka na tulivu zaidi katika kukimbia. Idadi ya timu zilizoshiriki iliongezeka hadi zaidi ya 100 mwaka huu, ikiwa ni pamoja na washiriki kutoka Ujerumani, Ufaransa na Brazili.
Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, roboti na wakimbiaji binadamu walifuata njia sawa lakini mistari tofauti ya kukimbilia ili kuhakikisha usalama, na muda wa roboti kuruhusiwa kumaliza mbio uliwekwa saa tatu na dakika 40. Mpangilio mpya ulioongezwa mwaka huu unajumuisha njia mbili za ushiriki – ukimbiaji wa kudhibitiwa kwa mbali na ule wa kujitegemea bila kudhibitiwa.
Kwa timu zilizokuwa katika ushiriki wa kudhibitiwa kutoka kwa mbali, muda wao wa kumalizia mbio unahitaji kuzidishwa kwa mgawo wa 1.2. Asilimia karibu 40 ya timu zilizoshiriki zilitumia njia ya kukimbia kwa kujitegemea ili kufikia matokeo mazuri.
Katika mashindano ya binadamu ya mbio za nusu marathon za E-Town, Zhao Haijie wa China alishinda taji kwa upande wa wanaume kwa kukimbia kwa saa moja, dakika saba, na sekunde 47, na mwenzake Wang Qiaoxia amekuwa mshindi katika mashindano ya mbio hizo kwa upande wa wanawake kwa kukimbia kwa muda wa saa 1:18:06.

Ndege wa Kwarara waingia msimu wa kuzaliana huko Shaanxi, China

Eneo la kaboni-sifuri katika Mkoa wa Hainan laonyesha vitendo vya kijani vya China

Vifaa vya kisasa vya usafi vyatoa huduma kwenye Mkutano wa Mwaka wa Jukwaa la Boao la Asia 2026

Eneo Jipya la Xiong'an la China labadilika kuwa mji wenye nguvu hai kutoka mpango
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
