Lugha Nyingine
China kutoza ushuru-sifuri kwa nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia
Idara ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali la China imetangaza jana Jumanne kuwa China itapanua utozaji ushuru-sifuri wa forodha kwa nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo kuanzia Mei 1, 2026.
Kwa mujibu wa tangazo hilo kuanzia Mei 1, 2026 hadi Aprili 30, 2028, China itatoza ushuru-sifuri wa forodha, katika mfumo wa viwango vya kodi vya upendeleo, kwa nchi 20 za Afrika ambazo zimeanzisha uhusiano wa kidiplomasia na China na haziainishwi kuwa ni nchi zenye maendeleo kidogo, hatua ambayo imeonesha azma ya China kupanua ufunguaji mlango wa kiwango cha juu.
Taarifa hiyo imesema kuwa, katika kipindi cha miaka miwili ya utekelezaji, China itaendelea kuhimiza mazungumzo na kusainiwa kwa makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya China na Afrika kwa Maendeleo ya Pamoja na nchi husika za Afrika.
Idara hiyo imeongeza kuwa hatua hiyo itachukua jukumu muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika vilevile kuendeleza juhudi za pamoja za kujenga jumuiya ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Katika taarifa, Wizara ya Biashara ya China imesema mpango huo wa ushuru-sifuri pia ni hatua bunifu na yenye vipindi huku China na nchi husika za Afrika zikifanya kazi kuelekea kusainiwa kwa Makubaliano ya Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya China na Afrika kwa Maendeleo ya Pamoja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



