Mkuu wa TAZARA apongeza makubaliano ya ufufuaji wa reli kuwa ni "mabadiliko makubwa"

(CRI Online) April 29, 2026

Kufufuliwa kwa Mamlaka ya Reli ya Tanzania-Zambia (TAZARA) kunaashiria mabadiliko makubwa katika historia ya reli hiyo, Mkurugenzi Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu mamlaka hiyo Bruno Ching'andu amesema, akibainisha kuwa mfumo wa makubaliano ya kuifufua ni "mabadiliko makubwa" ambayo yanashughulikia moja kwa moja changamoto za muda mrefu za ufadhili.

Reli ya TAZARA inaendelezwa kwa kiasi kikubwa chini ya mfumo wa makubaliano ya ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi baada ya kusainiwa kwa makubaliano na Kampuni ya Uhandisi wa Ujenzi ya China Septemba 29, 2025, ikikaribia maadhimisho ya miaka 50 tangu reli hiyo ianze shughuli zake za kibiashara yatakayofanyika mwaka 2026.

"Ingawa mahitaji ya huduma za reli kwenye njia hiyo yameendelea kuwa imara wakati wote, reli hiyo imekuwa ikikabiliwa na changamoto zisizoisha kutokana na mtaji mdogo wa uwekezaji katika miundombinu, vichwa vya treni, mabehewa, na mifumo ya kisasa ya uendeshaji.” Ching'andu amesema baada ya Mkutano na Maonesho ya hivi karibuni ya Zambia iliyounganishwa kwa Ardhi jana Jumanne.

Amesema mkataba huo unatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo wa TAZARA, kuboresha uhakika wa huduma, na kuimarisha jukumu lake la kuwa njia ya kimkakati ya biashara inayounganisha Bandari ya Dar es Salaam na Zambia na eneo pana la Kusini na Kati mwa Afrika.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha