Idadi ya vifo yaongezeka hadi 26 katika mlipuko wa kiwanda cha fataki katikati mwa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 06, 2026
Idadi ya vifo yaongezeka hadi 26 katika mlipuko wa kiwanda cha fataki katikati mwa China
Picha hii iliyopigwa Mei 5, 2026 ikionyesha hali ya sehemu inakofanyika shughuli ya uokoaji baada ya mlipuko katika kiwanda kimoja cha fataki huko Liuyang, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Chen Sihan)

CHANGSHA - Mlipuko uliotokea katika kiwanda kimoja cha fataki juzi Jumatatu katika Mkoa wa Hunan katikati mwa China umesababisha vifo vya watu 26 na wengine 61 kujeruhiwa, serikali ya mtaa ya huko imesema kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana Jumanne.

Chen Bozhang, meya wa Changsha, mji mkuu wa mkoa huo wa Hunan ametoa rambirambi kwa waathiriwa, na kuomba msamaha kwa familia zao, wakazi walioathiriwa, pamoja na jamii nzima.

"Tuna huzuni kubwa sana na tumejawa na majuto," amesema.

Kabla ya mkutano huo na waandishi wa habari kuanza, wahudhuriaji walikaa kimya kwa muda ili kutoa heshima kwa waathiriwa.

Mlipuko huo ulitokea saa 10:43 alasiri juzi Jumatatu katika kiwanda cha kampuni ya kutengeneza na kuonyesha fataki ya Huasheng huko Liuyang, mji wa wilaya wa Changsha, mji mkuu wa Hunan.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha