China yarekodi idadi kubwa ya safari za abiria kati ya mikoa wakati wa mapumziko ya Siku ya Mei Mosi (7)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 07, 2026
China yarekodi idadi kubwa ya safari za abiria kati ya mikoa wakati wa mapumziko ya Siku ya Mei Mosi
Treni ya mwendo-kasi ikipita katika eneo la mjini Kunming, Mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China, Mei 1, 2026. (Picha na Zheng Yi/Xinhua)

BEIJING – Jana Jumatano wizara ya mawasiliano na uchukuzi ya China imesema, idadi kubwa ya abiria waliofanya safari ya kutalii katika sehemu mbalimbali nchini China wakati wa mapumziko ya siku tano ya Tarehe Mosi, Mei, ambayo ni Siku ya Wafanyakazi Duniani imefikia rikodi mpya katika historia yake.

Wizara hiyo imesema kuwa, China ilirekodi safari za abiria takriban bilioni 1.52 katika sehemu mbalimbali nchini China wakati wa siku za mapumziko hayo, ambayo ni ongezeko la asilimia 3.49 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Wizara hiyo imesema, usafiri wa barabarani uliendelea kuwa njia kuu, ambapo safari ya watalii waliopanda magari ilifikia bilioni 1.39 ambayo ni ongezeko la asilimia 3.51 ikilinganisha na mwaka jana kipindi kama hicho.

Wizara hiyo imeeleza kuwa, usafirishaji wa abiria kwenye njia ya reli uliongezeka kwa asilimia 4.6, ambapo safari za abiria zilifikia milioni 106.38, wakati huohuo safari za abiria waliopanda meli zilishuka kwa asilimia 1.37 hadi milioni 8.49. Na safari za watu waliopanda ndege zilifikia milioni 10.54 katika kipindi hicho, ambayo ni idadi ya chini kwa asilimia 5.74 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.

Mawimbi ya usafiri wa watu wakati wa mapumziko ya Siku ya Mei Mosi nchini China yanachochewa zaidi na mahitaji makubwa ya utalii, kuwatembelea jamaa na marafiki na kufanya shughuli za burudani.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha