Lugha Nyingine
Hali inayovutia ya nyumba za kale katika Kijiji cha Baojing, Mkoa wa Hunan, China (2)
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 12, 2026
![]() |
| Picha iliyopigwa Mei 10, 2026 ikionyesha nyumba za kale katika Kijiji cha Baojing cha Yongzhou, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China. (Xinhua/Chen Zhenhai) |
Kijiji cha Baojing kilichoko sehemu ya milimani ya Wilaya Inayojiendesha ya Kabila la Wayao ya Jianghua huko Yongzhou, Mkoa wa Hunan, katikati mwa China kilijengwa na mababu wa Ukoo wa He mwaka 1650, na kwa hiyo kinaitwa "Nyumba za Ukoo He" (Courtyard of Family He). Mpaka sasa bado kuna mabaki ya nyumba za kale 180, minara 7 ya lango na vichochoro 36.
Kijiji hicho cha Baojing kiliwekwa kwenye kundi la nne la orodha ya vijiji vya jadi vya China mwaka 2016, na nyumba hizo za kale za Ukoo He ziliorodheshwa kuwa moja ya kundi la nane la mabaki muhimu ya kitamaduni ya ulinzi wa kitaifa mwaka 2019.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




