Lugha Nyingine
Umoja wa Mataifa wazindua mradi wa upanuzi kwenye makao makuu ya Nairobi, Kenya (4)
![]() |
| Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres (wa tano, kushoto) na Rais wa Kenya William Ruto (wa nne, kushoto) wakihudhuria hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya, Mei 11, 2026. (Xinhua/Yang Guang) |
NAIROBI - Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres na Rais wa Kenya William Ruto wamezindua mradi wa upanuzi wenye thamani ya dola milioni 340 za Marekani kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi (UNON).
Viongozi hao wawili waliongoza hafla jana Jumatatu ya kuweka jiwe la msingi kwa ujenzi wa mradi wa upanuzi wa majengo ya mikutano na ujenzi wa majengo ya ofisi ya kisasa zaidi yaliyo ya kuhimili mabadiliko ya tabianchi, na kuimarisha hadhi ya Nairobi ya kuwa kituo cha kidiplomasia katika Nchi za Dunia ya Kusini.
Mradi huo wa upanuzi wa UNON ulioidhinishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, unawekwa mkazo katika ujenzi wa majengo mapya ya ofisi ya kijani kwa dola milioni 66.2 na uboreshaji wa majengo ya mikutano kwa gharama ya dola milioni 265.7, na kuongeza idadi ya vyumba vya mikutano kutoka 14 hadi 30 na ujazo wa viti vya wajumbe vitaongezwa kutoka viti 2,000 hadi 9,000.
Mradi huo wa upanuzi utakapokamilika ifikapo mwaka 2029, utaiweka Nairobi katika nafasi ya kuwa kituo cha tatu kwa ukubwa cha Umoja wa Mataifa duniani baada ya New York na Geneva, huku Vienna ikibaki katika nafasi ya nne.
Rais Ruto amesema upanuzi huo wa ofisi za Umoja wa Mataifa jijini Nairobi unaendana na ahadi ya Kenya juu ya juhudi za pande nyingi zinazolenga kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa ya Umoja wa Mataifa na kuongeza uwezo wake wa kukabiliana na changamoto zinazowakabili binadamu.
"Ikiwa ni makao makuu pekee ya Umoja wa Mataifa katika Nchi za Kusini mwa Dunia, Nairobi ni alama yenye nguvu kwamba Umoja wa Mataifa hakika ni shirika la watu wa dunia nzima na linaonyesha matarajio ya pamoja ya binadamu," Rais Ruto amesema.
Katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Nairobi kuna ofisi za Mashirika zaidi ya 70 ya Umoja wa Mataifa, mifuko, na miradi, pamoja na wafanyakazi zaidi ya 6,000. Ruto amesema Kenya itawekeza katika ujenzi wa miundombinu ya uungaji mkono kama vile barabara, umeme, maji safi, usafi wa mazingira, afya, na usalama ili kuongeza uwezo wa utoaji huduma kwa watu wenye hali dhaifu zaidi katika eneo hilo. Kwa upande wake, Guterres amesema hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwa ujenzi wa ukumbi mpya wa mkutano na ujenzi wa majengo mapya ya ofisi vimeonesha ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kufanya juhudi za kuiweka Afrika kwenye kiini cha juhudi za baadaye za kuunda upya ushirikiano wa pande nyingi.
"Tunapoadhimisha miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Mataifa, tunafikiria upya namna tunavyofanya kazi, namna tunavyotoa huduma, na namna tunavyofanya uongozi. Tunafanya hivyo tukitambua jukumu la bara hili kubwa," Guterres amesema.
Guterres amesema mradi huo wa upanuzi pia umesisitiza ahadi ambayo taasisi za pande nyingi zitaleta huduma karibu zaidi na watu, wakati huohuo zitahimiza ushirikiano wa washirika wa kudumu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




