Lugha Nyingine
Ziara ya Utafiti ya Tovuti ya People’s Daily Online "China inayosonga Mbele" 2026 Yaanza huko Jiangxi
![]() |
| Ziara ya utafiti ya Tovuti ya People’s Daily Online “China inayosonga Mbele” 2026 ikianza huko Yudu, Jiangxi, China. (Picha na Zhu Haipeng/People’s Daily Online) |
Tarehe 11, Mei, Ziara ya Utafiti ya Tovuti ya People's Daily Online "China inayosonga Mbele" 2026 ilianza huko Yudu, mkoani Jiangxi.
Katika miaka zaidi ya 90 iliyopita, Jeshi Jekundu la Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China lilipiga hatua ya kwanza kutoka Yudu, likianza Safari Ndefu ya maili elfu kumi. Katika wakati wa mwaka huu ulio mwanzo wa utekelezaji wa Mpango wa 15 wa Miaka Mitano wa China na maadhimisho ya miaka 90 ya ushindi wa Safari Ndefu ya Jeshi Jekundu, Tovuti ya People’s Daily Online chini ya kaulimbiu ya "Kufanya Vizuri Safari Ndefu ya Zama Mpya" imeunda timu 31 za utafiti kwenda sehemu mbalimbali nchini kufanya utafiti kwa kupitia kazi za mwaka mzima za kukusanya habari na kufanya mahojiano, ili kuelezea vizuri simulizi za maendeleo ya China katika safari mpya, na kuonyesha hali mpya na mafanikio mapya ya makada na watu wa sehemu mbalimbali wanaopokezana majukumu katika hali mpya ya kihistoria kwa kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa yenye umaalumu wa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




