Lugha Nyingine
Wauguzi wa watoto wachanga wawaletea matumaini watoto wachanga katika Mkoa wa Yunnan, China
Yang Limei na wenzake ambao ni wauguzi wa watoto wachanga katika Hospitali ya Kwanza ya Mkoa wa Yunnan, kazi yao ya kila siku ni kutunza watoto wachanga wanaougua magonjwa hatari kama vile hali ya kuzaliwa njiti, hali ya kukosa hewa ya kutosha, magonjwa ya kuzaliwa nayo au hali ya kupatwa na maambukizi makali.
Ingawa maisha mapya kwa kawaida huwaletea watu furaha, lakini kufanya kazi za kuwaangalia watoto hawa wachanga katika hospitali hiyo kunamaanisha kutoa huduma kwa umakini zaidi na uangalifu mkubwa sana kwa Yang na wenzake. Wanahitaji kuwalisha watoto hao kila baada ya saa tatu, mara nane kwa siku, na kufuatilia bila kusita dalili muhimu ya afya ya watoto wachanga
Kuna wauguzi zaidi ya 60 kama Yang katika idara ya watoto wachanga ya hospitali hiyo. Katika miaka ya hivi karibuni, kila mwaka watoto wachanga zaidi ya 3,000 wamepona chini ya uangalizi wao. Hawa ndiyo wanaowaletea matumaini mwanzoni mwa maisha yao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




