Mkutano wa Ushirikiano wa China-Nchi za Kiarabu wa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Taasisi za Washauri Bingwa la Nchi za Dunia ya Kusini lafunguliwa Cairo (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 13, 2026
Mkutano wa Ushirikiano wa China-Nchi za Kiarabu wa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Taasisi za Washauri Bingwa la Nchi za Dunia ya Kusini lafunguliwa Cairo
Mkuu wa Shirika la Habari la China, Xinhua Fu Hua akimkabidhi Ahmed Aboul Gheit, katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, toleo la Kiarabu la kitabu cha Utawala wa China Chini ya Uongozi wa Xi Jinping kwenye makao makuu ya Ligi ya Nchi za Kiarabu, Cairo, Misri, Mei 12, 2026. (Xinhua)

CAIRO - Mkutano wa Ushirikiano kati ya China na Nchi za Kiarabu wa Jukwaa la Vyombo vya Habari na Taasisi za Washauri Bingwa la Nchi za Dunia ya Kusini umefunguliwa rasmi jana Jumanne kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu katika mji mkuu wa Misri, Cairo.

Shughuli hiyo ya siku mbili, chini ya kaulimbiu ya "Kuunganisha Hekima, Kuanza Safari Mpya: Kujenga Pamoja Jumuiya ya China na Nchi za Kiarabu yenye Mustakabali wa Pamoja," inakusanya wawakilishi wapatao 250 kutoka vyombo vya habari, taasisi za washauri bingwa, taasisi za serikali, kampuni kutoka China na nchi za Kiarabu takriban 110, vilevile mashirika ya kimataifa na ya kikanda.

Katika hotuba yake ya kufungua, Ahmed Aboul Gheit, katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, amesema kwamba nchi za Kusini mwa Dunia zinakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Amesema Pendekezo la Uongozi Duniani lililopendekezwa na Rais wa China Xi Jinping, limefungua matarajio mapana ya kuhimiza demokrasia katika uhusiano wa kimataifa, kupunguza pengo kati ya nchi za Dunia ya Kaskazini na Kusini, kutatua migogoro duniani kwa njia za amani, na kujenga mustakabali bora pamoja.

Amesisitiza kwamba vyombo vya habari na taasisi za washauri bingwa za nchi za Kiarabu na China zinahitaji kuimarisha ushirikiano haraka, kujenga maafikiano, kuhimiza uhusiano imara kati ya watu wa nchi za Kiarabu na China, na kuhimiza utaratibu wa kimataifa wenye haki na usawa zaidi.

Mkuu wa Shirika la Habari la Xinhua la China, Fu Hua, kwa upande wake, amesema kwamba chini ya mwongozo wa kimkakati wa Rais Xi na viongozi wa nchi za Kiarabu, uhusiano kati ya China na nchi za Kiarabu umeingia katika kipindi chake bora zaidi katika historia: kuaminiana kimkakati kumezidishwa kwa kasi, ushirikiano katika nyanja mbalimbali umeendelea kupanuka, na mabadilishano ya kati ya watu na watu na ya kitamaduni yametoa matokeo mazuri.

Katika hotuba yake, Balozi wa China nchini Misri Liao Liqiang amesema kwamba miaka 10 iliyopita, Rais Xi alifanya ziara kwenye makao makuu ya Umoja wa Nchi za Kiarabu na kutoa hotuba muhimu katika ukumbi huu, akitoa jibu la China kwa "suala la Mashariki ya Kati," akisisitiza kwamba kulikumbuka leo kunalifanya liwe lenye kuelekeza zaidi.

"Si muda mrefu uliopita, Rais Xi alitoa pendekezo la pointi nne juu ya kulinda na kuhimiza amani na utulivu katika Mashariki ya Kati, ambalo limepokea uungaji mkono mpana na mwitikio mzuri kutoka kwa jumuiya ya kimataifa," Liao ameongeza.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha