Lugha Nyingine
Rais wa Afrika Kusini atoa wito wa kuimarisha ushirikiano katika shughuli za utalii barani Afrika katika Travel Indaba 2026 (7)
![]() |
| Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akihutubia hafla ya kufunguliwa kwa Mkutano wa Utalii wa Afrika 2026, (Africa’s Travel Indaba 2026) jijini Durban, Afrika Kusini, Mei 12, 2026. (Xinhua/Chen Wei) |
DURBAN - Mkutano wa Utalii wa Afrika 2026 (Africa’s Travel Indaba 2026) umeanza rasmi Jumanne wiki hii nchini Afrika Kusini, ambapo Rais Cyril Ramaphosa ametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa bara hilo ili kufungua nguvu bora za shughuli za utalii ambazo ni kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi barani Afrika.
"Kwa nchi nyingi za Afrika, shughuli ya utalii si tu shughuli ya mapumziko, bali pia ni chombo ambacho kwa kukitumia tunaweza kukuza uchumi wetu," Rais Ramaphosa amesema kwenye hafla ya kufungua shughuli hiyo katika jiji la pwani la Durban
Rais Ramaphosa amesema Afrika Kusini iliwapokea watalii milioni 10.5 wa duniani mwaka 2025, huku robo tatu ya watalii hao waliowasili wakitoka eneo la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Ametoa wito wa kuendeleza kwa kina zaidi utandawazi wa shughuli za utalii barani Afrika, akisema Afrika Kusini inashirikiana na nchi jirani katika kusukuma mbele mpango wa urahisishaji wa visa za utalii katika eneo la SADC (SADC Tourism UNIVISA), ambao unalenga kuwezesha safari za utalii zisizo na vizuizi katika nchi wanachama.
Amesema mpango huo una malengo sawasawa na malengo mapana ya Ajenda ya Umoja wa Afrika ya 2063 na Eneo la Biashara Huria la Bara la Afrika, yote hayo yakilenga kuhimiza mzunguko huria zaidi wa watu na kuimarisha zaidi mahusiano ya biashara na uwekezaji ya sehemu mbalimbali barani Afrika.
"Tunapotazama mustakabali wa siku za baadaye, lazima tuendelee kupanua chanzo cha masoko yetu," Ramaphosa amesema, akisema kuwa Afrika Kusini inaongeza juhudi za kuvutia watalii kutoka masoko yanayokua kwa kasi kama vile ya China, India, Asia Kusini-Mashariki, Mexico na Brazil.
Ameongeza kuwa mageuzi ya visa, ikiwemo mfumo wa Uidhinishaji wa Msafiri Kielektroniki na Visa ya Digital Nomad, yanalenga kufanya usafiri wa kwenda Afrika Kusini "kuwa rahisi zaidi bila vizuizi."
Mkutano huo wa Utalii wa Afrika (Africa’s Travel Indaba), ni maonyesho ya biashara ya utalii wa mapumziko ambayo ni alama ya Afrika, na yanayomilikiwa na Mamlaka ya Utalii ya Afrika Kusini kwa lengo maalum la kujenga ufikiaji wa soko kwa bidhaa nyingi za utalii wa mapumziko wa Afrika.
Maonesho hayo ya siku tatu ya mwaka huu, yanayofanyika chini ya kaulimbiu ya "Afrika Isiyo na Vizuizi: Kukuza Uchumi wa Utalii wa Afrika," yamevutia waonyeshaji zaidi ya 1,200 kutoka nchi 22 za Afrika na wanunuzi karibu 1,000 kutoka nchi 44.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




