Lugha Nyingine
Timu ya wahifadhi vijana yatumia teknolojia ya kisasa kwa kuhifadhi sanaa ya michongo ya mawe ya dini ya Kibuddha (6)
Katika Taasisi ya Mapango ya Longmen ya Mkoa wa Henan katikati mwa China, timu ya vijana wachapa kazi inabeba jukumu la kuhifadhi na kufuatilia Mapango ya Longmen, Eneo la Mali ya Urithi ya Dunia kwenye orodha ya UNESCO, kwa kutengeneza makavazi ya kidijitali ya michongo ya mawe ya dini ya Kibuddha.
Tokea mwaka 2005, taasisi hiyo ya Mapango ya Longmen ilianza kufanya kazi ya kuskani kwa kutumia leza na upigaji picha za hali ya juu ili kuhifadhi kidijitali sanaa za michongo ya mawe za China zenye historia ya miaka 1,500.
Katika miaka ya hivi karibuni, timu hiyo imeongoza miradi nyingi ya ukarabati na uhifadhi wa mabaki ya kale ya kitamaduni ya ngazi ya kitaifa na ya mkoa na kuchangia katika uhifadhi na ufuatiliaji wa mali muhimu ya urithi wa kitamaduni ikiwa ni pamoja na Njia ya Kale ya Hariri na Mfereji Mkuu wa Sui (581-618) na enzi za Tang (618-907).
Timu hiyo imepewa Nishani ya Vijana ya Mei Nne ya China ya mwaka huu, ambayo ni heshima ya juu zaidi ya nchi inayotolewa kwa vijana.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




