Wilaya ya Qimen, Mashariki mwa China yafanya uboreshaji wa kidijitali wa   shughuli za chai nyekundu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 20, 2026
Wilaya ya Qimen, Mashariki mwa China yafanya uboreshaji wa kidijitali wa   shughuli za chai nyekundu
Picha ikionyesha wafanyakazi wakikagua zana za kufuatilia wadudu kwa kutumia teknolojia ya AI kwenye bustani ya chai ya kielelezo cha kiikolojia katika Wilaya ya Qimen ya Mji wa Huangshan, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Mei 16, 2026. (Picha na Fan Chengzhu/Xinhua)

Katika miaka ya hivi karibuni, Wilaya ya Qimen katika Mji wa Huangshan, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, ambayo ni maarufu sana kwa chai yake nyekundu, imefanya uboreshaji wa kidijitali wa shughuli zake za chai.

Ikiwa sehemu moja ya juhudi hizo, vitambuzi janja vimewekwa kwenye bustani za chai ili kufuatilia mabadiliko ya hali ya hewa na unyevunyevu wa udongo kwa wakati halisi, wakati huohuo mifumo nyunyizi ya umwagiliaji inatoa maji kadiri inavyohitajika na kuunga mkono udumishaji sahihi zaidi wa hali hitajika. Wilaya hiyo pia imekuwa ikitumia droni kubeba majani freshi ya chai yaliyochumwa punde katika muda wa dakika chache tu, na kuongeza ufanisi zaidi wa usafirishaji.

Zaidi ya hayo, Wilaya ya Qimen imeboresha mnyororo mzima wa uzalishaji wa chai nyekundu kwa kuingiza mistari jumuishi ya uzalishaji ya kutumia teknolojia ya AI ili kuhakikisha uzalishaji sanifu. Uboreshaji huo unasaidia chai nyekundu ya Qimen kupanua soko la ng'ambo na kuongeza zaidi nguvu ya ushindani duniani ya chai hiyo nyekundu ya China.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha