Eneo la viwanda vya kidijitali yaongeza uwezo wa viwanda vya teknolojia ya AI vya Tianjin (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2026
Eneo la viwanda vya kidijitali yaongeza uwezo wa viwanda vya teknolojia ya AI vya Tianjin
Wahandisi wakirekebisha roboti kwenye kampuni ya teknolojia ya SYNROX katika kiwanda cha 764 cha Aerospace, huko Tianjin, kaskazini mwa China, Mei 20, 2026. (Xinhua/Sun Fanyue)

Kiwanda cha 764 Aerospace kiko kwenye sehemu ya zamani ya kiwanda cha kitaifa cha zana na vifaa vya radio, sasa sehemu hiyo ni eneo la viwanda vya kidijitali katika Eneo la Hexi la Tianjin, China, ambapo kuna viwanda zaidi ya 10 vya teknolojia za hali ya juu.

Sifa zaidi ya viwanda vya eneo hilo ni kutumia teknolojia ya AI kwa kuweka mkazo zaidi katika kusukuma mbele ukusanyaji wa data za AI, kufanya marekebisho na majaribio ya roboti, kufanya Utafiti na Maendeleo ya algoriti na matumizi katika mazingira mahsusi, na vimejenga kundi la mnyororo kamili wa viwanda unaohusisha mchakato mzima kuanzia ukusanyaji wa data hadi upangaji wa kazi katika mazingira mahsusi.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha