Habari picha ya vinywaji vya chai vya mtindo wa China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 22, 2026
Habari picha ya vinywaji vya chai vya mtindo wa China
Kikombe cha kinywaji kipya cha chai cha mtindo wa China kilichotengenezwa na Wang Sun kikionyeshwa kwenye shule ya ufundi stadi wa kazi ya kuonesha utamduni wa chai ya Demingshe katika Mji wa Huangshan, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Aprili 24, 2026. (Picha na Shi Yalei/Xinhua)

Katika Mji wa Huangshan, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, ambao ni chimbuko la aina maarufu za chai za Huangshan Maofeng, Taiping Houkui na Chai Nyekundu ya Qimen, vinywaji vya chai vya mtindo wa China vimekuwa mtindo wa aina mpya katika miaka ya hivi karibuni.

Wang Sun, ambaye alianzisha shule ya ufundi stadi wa kazi ya kuonesha utamaduni wa chai ya Demingshe katika mji huo wa Huangshan, amekuwa akiongoza utafiti na utangazaji wa vinywaji vya chai vya mtindo wa China tokea mwaka 2021.

Chapa za vinywaji vya chai vinavyounganisha chai na dawa za jadi za mitishamba ya China zimekaribishwa na vijana kutokana na kulingana na mahitaji yao ya mtindo wa maisha yanayosaidia afya.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha