Lugha Nyingine
Habari picha: mpanga safari za watalii wanaoingia China awaonyesha hali halisi ya Shanghai (6)
![]() |
| Liu Lichao akiwaongoza wateja wake kutembelea Bustani ya Fuxin mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 16, 2026. (Xinhua/Chen Haoming) |
Wakati huu ambapo tangazo la "Fanya Utalii China" likijulikana zaidi kwenye majukwaa ya mitandao ya kijamii duniani, shughuli za utalii zinazowavutia watalii wa nje kuja China zimeendelea kuonesha hali ya ustawi mzuri, na mji wa Shanghai umekuwa kituo cha kwanza kwa watalii wa ng'ambo.
Liu Lichao alipofanya kazi ya mambo ya fedha aligundua kitu kisichotarajiwa wakati yeye na wateja wake wa ng'ambo wakiendesha baiskeli kutembelea mitaani pamoja, aliona watu kutoka nchi mbalimbali zenye tofauti ya utamaduni huwa wanaweza kuonekana kuwa na raha na wepesi zaidi, na hali hii hufanya mawasiliano kati yao kuwa rahisi zaidi.
Mwaka 2024, Liu aliacha kazi yake ya awali na kuanza kuwa mpanga rasmi wa safari za watalii wanaoingia China kutali, akipangilia safari mahsusi za utalii zinazowawezesha watalii kutoka nchi mbalimbali duniani wajionee hali halisi ilivyo ya miji ya China.
Kwa Liu, kuendesha baiskeli kutembelea mitaani pamoja na watalii kutoka nje ni njia bora ya kuwaonyesha hali halisi ya Shanghai. Kila mara aliwaongoza wateja wake kutembelea kwenye eneo la zamani la kimahaba la French Concession, vichochoro vyenye historia ndefu mjini humo, na majengo ya kifahari yenye bustani kando ya Barabara ya Nanchang, pia aliwaongoza kwenda migahawa inayotoa vyakula freshi mbalimbali vinavyofurahisha watu.
Liu hapendi kuwaongoza watalii kupita haraka sehemu zilizo za alama za mji na zenye vivutio, badala yake anafurahia kuendesha baiskeli pamoja na wateja wake kutembelea mitaani huku akiwaelezea hali na vitu walivyojionea na kuwavutia njiani.
"Hayo ni mawasiliano kati yetu kuhusu utamaduni wa pande mbilimbili," Liu amesema, akiongeza, "Ninachotaka kuonyesha ni upande halisi na wa kila siku wa nchi yangu."
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




