Lugha Nyingine
Visa zaidi ya 900 vinavyoshukiwa vyatambuliwa katika kukabiliana na Ebola DRC: Mkuu wa WHO (2)
GENEVA - Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema kwamba huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ikiongeza ufuatiliaji katika kukabiliana kwake na Ebola, visa zaidi ya 900 vinavyoshukiwa vimetambuliwa hadi sasa, ikiwa ni pamoja na visa 101 vilivyothibitishwa.
Katika Jimbo la Ituri, eneo lililoathirika zaidi na mlipuko huo, watu karibu milioni 5 wanaishi katikati ya mgogoro unaoendelea, huku mmoja kati ya wanne akihitaji msaada wa kibinadamu na mmoja kati ya watano wakiwa wamekimbia makazi yao, Tedros alisema Jumapili katika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X.
"Vurugu zinalazimisha watu kukimbia, wakiwemo wafanyakazi wa afya na wa kibinadamu. Hii inatatiza vikali juhudi za kuongeza ufuatiliaji wa watu waliokabiliwa na walioambukizwa Ebola na kutambua maambukizi mapema kutosha kutoa huduma ya uungaji mkono," ameongeza, akibainisha kuwa hali inayoendelea ya ukosefu wa usalama na hofu pia inachochea kutoaminiana ndani ya jamii.
Mkuu huyo wa WHO amesema kwamba WHO na washirika wa afya ya kibinadamu wanadumisha uwepo kote Ituri, ikiwemo katika baadhi ya maeneo magumu kufikiwa na yasiyo salama, ambako jamii zinakabiliwa na si tu tishio la Ebola bali pia magonjwa mbalimbali.
Tedros amesisitiza kwamba kutoa kifurushi kamili cha huduma za afya ni muhimu -- si tu kukidhi mahitaji ya dharura ya kiafya, bali pia kujenga kuaminiana ambako ni muhimu kwa kukabiliana ipasavyo na Ebola.
Mei 16, Tedros aliamua kwamba ugonjwa huo wa Ebola unaosababishwa na virusi vya Bundibugyo nchini DRC na Uganda ni dharura ya afya ya umma inayohitaji umakini na ufuatiliaji wa kimataifa.
Mei 22, WHO ilirekebisha tathmini yake ya hatari hadi kuwa ya "juu sana" katika ngazi ya kitaifa, huku ikiiweka "juu" katika ngazi ya kikanda na "chini" duniani kote.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




