Lugha Nyingine
Madaraja ya matao yenye mapaa ya mbao yahifadhiwa vizuri katika Mkoa wa Fujian, China (5)
![]() |
| Picha hii iliyopigwa Mei 14, 2026 ikionyesha hali ya ndani ya Daraja la Xiangong katika Wilaya ya Shouning ya Mji wa Ningde, Mkoa wa Fujian, kusini mashariki mwa China. (Xinhua/Wei Peiquan) |
Daraja la matao lenye paa la mbao ni muundo wa kikale wa kipekee, ambao sifa yake ni korido inayojengwa juu ya daraja la kuvuka mto. Madaraja ya aina hiyo yanaonyesha ufundi stadi wa hali ya juu wa wajenzi wa zama za kale waliounganisha mbao kwenye tao bila kutumia misumari au vipuri vya madini.
Katika Mkoa wa Fujian kuna madaraja 547 ya aina hiyo. Mkoa huo umeweka mkazo katika ulinzi na urithi wa ufundi huo wa ujenzi wa daraja. Umechukua hatua za kivumbuzi ikiwa ni pamoja na bima ya mabaki ya kale ya kitamaduni, ufuatiliaji kwa kutumia AI, na raslimali mpya za uhifadhi kwa ajili ya ukaguzi na matengenezo ya mara kwa mara juu ya madaraja hayo, na thamani ya uwekezaji katika kazi hizo imefikia yuan jumla ya milioni 61.03 (dola za Marekani karibu milioni 8.93).
Mwezi Desemba mwaka 2024, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliuweka usanifu wa kijadi na ufundi wa kujenga madaraja hayo ya China kwenye Orodha yake ya Uwakilishi wa Urithi wa Utamaduni Usioshikika wa Binadamu.
Ili kuhimiza urithi na maendeleo ya kivumbuzi ya madaraja hayo ya kale, mkoa huo wa Fujian umefanya juhudi za kuanzisha kazi ya kufanya mafungamano ya utamaduni na utalii, wakati huohuo kuwaandaa warithi wenyeji wa ufundi huo wa kijadi wa kujenga madaraja.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




