Lugha Nyingine
Njia maalum ya basi ya kuwahudumia wakulima yaanzishwa katika Kijiji cha Jiaxi mkoa wa Jiangxi, China (5)
![]() |
| Watu wakipanda basi mahsusi kwenye kituo cha basi katika Kijiji cha Jiaxi cha Mji mdogo Xiangtang wa Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China, Mei 9, 2026. (Xinhua/Wan Xiang) |
Katika Kijiji cha Jiaxi cha Mji mdogo Xiangtang wa Nanchang, Mkoa wa Jiangxi, mashariki mwa China, wakulima wengi kama alivyofanya Jiang Changhua wanategemea kuuza mboga freshi kama chanzo chao kikuu cha kupata kipato. Wakulima katika kijiji hicho walikuwa wakihangaika kubeba mizigo mizito hadi soko la mjini, kazi ambayo ilichukua muda mrefu na kuwachosha sana kwa sababu kijiji chao kiko mbali na Mji Nanchang na walikuwa hawakuweza kupata usafiri kirahisi.
Ili kutatua tatizo hilo, serikali ya mitaa na kampuni ya mabasi ya umma zimeanzisha njia maalum ya basi ya kuwahudumia wakulima hao, ikiwawezesha wanakijiji kwenye kando za njia hiyo kupata urahisi kwenda mjini na kuuza mazao yao freshi. Sasa Jiang huamka mapema saa 9 alfajiri ili kwenda shambani kuchuma mboga zake na kuzibeba hadi kwenye kituo cha basi. Wahudumu wa kituo cha basi na ndani ya basi wanaweza kuwasaidia kuweka vikapu vya mboga ndani ya basi na kuhifadhi hali ya utaratibu.
Kutokana na huduma hiyo mahsusi ya basi, wakulima wanaweza kuleta mboga freshi zilizochumwa asubuhi mapema kwenda soko la mjini, kuziuza haraka na kupata kipato zaidi.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




