Lugha Nyingine
Meli kubwa ya kitalii ya pili kuundwa ndani ya China yakamilisha jaribio la kwanza la baharini
![]() |
| Meli ya kitalii ya Adora Flora City ikiwa imetia nanga kwenye bandari mjini Shanghai, mashariki mwa China, Mei 27, 2026. (Xinhua/Fang Zhe) |
SHANGHAI - Meli kubwa ya kitalii ya pili iliyoundwa ndani ya China, Adora Flora City, imerudi bandarini mjini Shanghai jana Jumatano baada ya kukamilisha jaribio la kwanza la siku 12 ya baharini, ikiashiria hatua muhimu katika juhudi za nchi hiyo za kuzalisha meli kubwa za kitalii kwa wingi.
Timu ya wataalamu 937 kutoka nchi 12 imekamilisha upimaji ufanisi na kazi za uthibitishaji 149 wakati wa jaribio hilo, ikitathmini uwezo wa meli hiyo kufanya mambo mbalimbali, mifumo ya otomatiki, usalama na ubora wa huduma, na ufanisi wa utoaji hewa chafu, ulitangaza muundaji wa meli hiyo, Shirika la Uundaji Meli la China (CSSC).
Alessio Pinizzotto, meneja mradi katika kampuni ya kimataifa ya Italia Registro Italiano Navale (RINA), amesema RINA imefuata taratibu zote muhimu za upimaji kwa meli hiyo na amekielezea chombo hicho kuwa ni "meli yenye ushindani mkubwa" katika soko la Asia.
"Vigezo vyote vya matumizi na mazingira vimepangwa sawia, na muhimu zaidi, hali ni hiyohiyo kwa usalama," Pinizzotto amesema, akiongeza kuwa meli hiyo imeundwa kwa muda mfupi kwa kutumia teknolojia ya hali ya juu.
"Hii inaonyesha kuwa yadi hii ya meli ina nguvu bora kubwa zaidi za kukua na kuwa na ushindani katika tasnia ya meli za kitalii duniani," Pinizzotto amebainisha.
Meli hiyo imekamilisha vitu vyote vya jaribio vinavyohitajika katika safari moja, ikilinganishwa na majaribio mawili ya baharini kwa meli kubwa ya kitalii ya kwanza kuundwa ndani ya China, Adora Magic City, ikiashiria hatua zaidi mbele katika uwezo wa China katika uundaji wa meli kubwa za kitalii.
Chen Gang, kamanda mkuu wa jaribio hilo la baharini, amesema jaribio hilo limeenda vizuri na limeweka msingi imara kwa meli hiyo kuwasilishwa kwa mteja kwa wakati uliopangwa.
Ameeleza kuwa, jaribio hilo lenye mafanikio liliungwa mkono na wataalamu, timu ya kimataifa ya usimamizi wa uhandisi, vilevile maboresho ya kimfumo katika usimamizi wa mnyororo wa ugavi na upangaji wa miradi.
Meli hiyo imepangwa kuwasilishwa kwa mteja Novemba 6 na itaendeshwa kwenye njia za kimataifa kutoka Bandari ya Kimataifa ya Meli za Kitalii ya Nansha mjini Guangzhou, mji mkuu wa Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




