Vifo kutokana na ajali ya moto katika shule ya Kenya vyaongezeka hadi 16 (8)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2026
Vifo kutokana na ajali ya moto katika shule ya Kenya vyaongezeka hadi 16
Mtu akipiga picha ya eneo la Shule ya Wasichana ya Utumishi, baada ya kutokea kwa ajali ya moto, Gilgil, Kaunti ya Nakuru, Kenya, Mei 28, 2026. (Xinhua/Yang Guang)

GILGIL – Polisi nchini Kenya wamethibisha jana Alhamisi kwamba idadi ya vifo vya watu kutokana na ajali ya moto iliyotokea mapema asubuhi kaskazini magharibi mwa Kenya imeongezeka hadi kufikia 16 baada ya wanafunzi wengine sita kufariki dunia kwa sababu ya kujeruhiwa vibaya.

Moto huo ulizuka majira ya saa 7:00 usiku wa kuamkia Alhamisi kwa saa za Afrika Mashariki (2200 GMT Jumatano) wakati wanafunzi walikuwa wamelala bwenini katika Shule ya Wasichana ya Utumishi huko Gilgil, Kaunti ya Nakuru, na hapo awali ilitangazwa kwamba ulikuwa umesababisha vifo vya watu 10 kabla ya idadi hiyo kuongezeka.

Wakati huo huo, watu zaidi ya 70 wanaendelea kulazwa hospitalini wakiwa na majeraha ya hali mbalimbali tofauti. Ripoti hiyo ya polisi imesema kwamba watu wengi waliojeruhiwa kwa sasa wako katika hali nzuri.

Chanzo cha ajali hiyo ya moto bado kinaendelea kuchunguzwa.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha