ChinaVumbuzi |  Maonyesho ya AI Duniani yasisitiza ufungamanishaji wa viwandaviwanda vya AI, ushirikiano wa kimataifa (6)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Mei 29, 2026
ChinaVumbuzi |  Maonyesho ya AI Duniani yasisitiza ufungamanishaji wa viwandaviwanda vya AI, ushirikiano wa kimataifa
Watu wakitazama vitu vinavyooneshwa vinavyohusiana na uchumi wa anga ya chini kwenye Maonyesho ya AI Duniani 2026, Tianjin, kaskazini mwa China, Mei 28, 2026. (Xinhua/Sun Fanyue)

TIANJIN - Maonyesho ya AI Duniani 2026 yameanza rasmi jana Alhamisi katika Mji wa Tianjin kaskazini mwa China, yakiwaleta pamoja waonyeshaji zaidi ya 700 kuonyesha teknolojia za kisasa za hali ya juu, bidhaa na matumizi halisi kwenye mazingira mbalimbali katika nyanja ya akili bandia (AI).

Maonyesho hayo ya siku nne yaliyoandaliwa kwa pamoja na serikali za mji huo wa Tianjin na ule wa Chongqing kusini magharibi mwa China, yanafanyika chini ya kaulimbiu ya "AI: Nafasi Kubwa ya Maendeleo, Kichocheo cha Ukuaji Endelevu." Yana maeneo saba ya maonyesho yanayojumuisha roboti za AI za maumbo, teknolojia kuu za AI, uchumi wa anga ya chini na utafiti wa anga ya juu wa kibiashara, yakiwa na eneo lenye ukubwa wa jumla wa mita za mraba 130,000

Kwa mujibu wa waandaaji hao, maonyesho hayo yamevutia kampuni ongozi, zikiwemo kampuni 500 Bora Duniani (Fortune Global 500 firms) na kampuni za juu kabisa za China katika sekta ya AI.

Ufungamanishaji wa AI viwandani unaharakishwa, kuchochea uboreshaji wa ufanisi katika sekta za kawaida na kujenga mifumo mipya ya biashara, wamesema wadau wa viwandaviwanda hivyo wanaohudhuria maonyesho hayo.

Naibu waziri wa viwanda na teknolojia ya kupashana habari wa China Ke Jixin amesema wizara hiyo itafanya kazi na pande zote ili kuhimiza maendeleo ya ubora wa juu ya viwanda vya AI, kusukuma mbele mpango wa "AI+ viwanda", kuimarisha uwezo wa uvumbuzi na kuboresha mazingira ya viwanda.

Liu Liehong, mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Data ya China, amebainisha kuwa seti za data zenye ubora wa hali ya juu hutumika kama rasilimali ya kiufundi na pia injini ya uvumbuzi kwa ajili ya uboreshaji wa AI wa viwanda vya hali ya juu.

"Tunawaunga mkono kampuni ongozi na vyombo vya majaribio katika uzalishaji bidhaa viwandani ili kujenga seti za data zenye ubora wa hali ya juu katika maeneo muhimu, yakiwemo uundaji wa magari, ujenzi wa meli, usafiri wa reli, metali na petrokemikali," Liu ameongeza.

Kadri nchi nyingi zinavyotaka kuwezesha viwanda kupitia AI, China inahimiza kwa juhudi kubwa ushirikiano wa kimataifa katika nyanja hiyo.

"Tunaifanya AI kuwa kipaumbele katika ushirikiano wa teknolojia wa pande mbili na pande nyingi. Tutazidisha ushirikiano wa kimataifa juu ya AI na kuimarisha uvumbuzi wa kiteknolojia na ujengaji uwezo," amesema Chen Jiachang, naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China.

Hussain bin Ibrahim Al Hammadi, Balozi wa Falme za Kiarabu nchini China, ameelezea matarajio yake ya ushirikiano. Amesema mbinu ya China ya kutumia teknolojia kuboresha maisha ya watu inaendana vyema na maono ya UAE ya kujenga uchumi wa kivumbuzi na unaotegemea maarifa ambao unatilia maanani mustakabali wa siku za baadaye.

Maonyesho hayo yataendelea hadi Jumapili. Wakati wa shughuli hiyo, bidhaa mpya zaidi ya 200, teknolojia, mafanikio na ripoti za utafiti zitatolewa, zikijumuisha roboti za AI zenye maumbo, magari yaliyounganishwa kwa AI, uchumi wa anga ya chini, uzalishaji bidhaa kwa kutumia AI na maisha ya kutumia teknolojia janja.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha