Lugha Nyingine
Mrithi wa mali ya urithi ya Mkoa wa Xizang wa China ajitolea kueneza Duixie (7)
Nyima Tsamjo ni mrithi wa mali ya urithi wa utamaduni usioshikika wa ngazi ya kimji katika Mkoa Unaojiendesha wa Xizang, kusini magharibi mwa China anayebobea katika "Duixie", sanaa ya nyimbo na ngoma ya kijadi ya kabila la Watibet yenye historia ya tangu enzi na dahari.
Tangu alipokuwa utotoni amesoma na kufanya mazoezi ya sanaa hiyo ya kuimba nyimbo na kucheza ngoma, na shauku yake kwa "Duixie" haijawahi kupungua hata kidogo.
"Duixie" ikiwa ni aina ya sanaa inayowakilisha kiwango cha juu katika maendeleo ya sanaa za maonesho za kijadi za kabila la Watibet, umependwa sana na watu hasa katika maeneo ya miji ya kitibeti ikiwa ni pamoja na miji ya Lhasa na Xigaze katika mamia ya miaka iliyopita.
Tangu mwaka 2007, Nyima Tsamjo amekuwa akijitolea kwa nguvu zote katika shughuli za kurithisha mali ya urithi wa "Duixie" zisizotaka faida. Amekuwa akisafiri katika sehemu nyingi za Xizang kufanya madarasa ya umma bila malipo, akishikilia kukaa kwenye mstari wa mbele wa kutoa mafunzo mwaka mzima, na wanafunzi wa rika zote wamesoma katika madarasa yake hayo ya umma.
Mwaka 2013, "Duixie" ya Lhasa, ambayo ni mali ya urithi maalum aliourithisha, uliorodheshwa kuwa moja ya kundi la nne la urithi wa utamaduni usioshikika wenye ulinzi wa ngazi ya mkoa huo unaojiendesha.
Hivi sasa Nyima Tsamjo amekuwa na umri wa miaka 60, lakini bado anachukua utoaji mafunzo ya "Duixie" kuwa ni wajibu wake, na ameongeza nguvu hai ya urithi wa utamaduni huo wa kale usioshikika wa sanaa ya nyimbo na ngoma.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




