Lugha Nyingine
Uhifadhi wa tumbili macaque kusini-magharibi mwa China wapata maendeleo (7)
![]() |
| Picha iliyopigwa Mei 31, 2026 ikiwaonesha tumbili macaques wakiwa kwenye eneo la vivutio vya utalii la Magenge Matatu Madogo katika Wilaya ya Wushan, huko Chongqing, kusini magharibi mwa China, Mei 31, 2026. (Xinhua/Huang Wei) |
CHONGQING – Tumbili Macaque ni wanyama wa uhifadhi wa kitaifa wa ngazi ya pili nchini China. Katika wakati wa mwaka 2000 hivi, shughuli za ukataji miti na uchimbaji wa ardhi kwa kilimo, eneo la makazi asilia ya wanyama pori lilipungua, na kusababisha idadi ya wanyama hao ilipungua hadi chini ya 100 katika eneo la Magenge Matatu Madogo.
Serikali ya mitaa ya huko ilihamisha wakazi kutoka sehemu muhimu za makazi ya wanyamapori, iliondoa magati yaliyokuwa sehemu za kawaida tumbili macaque walipokusanyika, na kuanzisha kazi ya upandaji miti kwenye sehemu kubwa. Leo hii, tumbili macaque pori wapatao elfu kadhaa wanaishi katika eneo hilo.
Kadri idadi ya tumbili hao macaque ilivyozidi kuongezeka, upatikanaji chakula milimani ulianza kuwa usiotosheleza. Ili kupunguza migogoro kati ya tumbili macaque na watu wa sehemu za makazi zilizo karibu, serikali ya mitaa iliweka sehemu nne za kuwalisha wanyama chakula, ambapo wafanyakazi huwapa tumbili hao mahindi mara kwa mara.
Gong Qingbing amekuwa akijishughulisha na ulishaji wa tumbili macaque kwa miaka 22. Miluzi ya filimbi anayopiga imekuwa ishara inayofahamika sana kati yake na tumbili hao macaque. "Natumai milima itakuwa kijani zaidi na maji kuwa safi zaidi, na tumbili macaque na wakazi wenyeji wanaweza kuishi maisha bora," Gong amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




