Mabadilishano ya kati ya watu na watu ya China na Marekani yapata kasi (3)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 02, 2026
Mabadilishano ya kati ya watu na watu ya China na Marekani yapata kasi
Christopher Nixon Cox, mjukuu wa Rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon, akizungumza kwenye Hafla ya Miaka 100 tangu kuanzishwa Taasisi ya China ya Amerika jijini New York, Marekani, Mei 28, 2026. (Picha na Zack Zhang/Xinhua)

NEW YORK - Huku Taasisi ya China ya Amerika, shirika lisilo la faida linalojitolea mahsusi kwa ajili ya kuzidisha uelewa wa China, ikisherehekea miaka yake 100 tangu kuanzishwa kwake, washiriki kutoka taasisi mbalimbali na wawakilishi wa familia za marais wa zamani wa Marekani wamepaza sauti kuunga mkono ushiriki na mabadilishano ya kati ya watu na watu ya Marekani na China.

Christopher Nixon Cox, mjukuu wa Rais wa zamani wa Marekani Richard Nixon, amesema kwamba akikabiliwa na tofauti kati ya China na Marekani, babu yake "aliahidi kitu fulani kigumu na cha udhati zaidi, daraja la kusimama na kuzungumza."

“Somo la mwaka 1972 ni kwamba hata baada ya miongo kadhaa ya ukimya, hata katika pande za ghuba yenye kina zaidi, watu wenye nia njema wanaweza kupata njia ya kuzungumza na kuivuka," amesema Cox, akikumbushia ziara muhimu ya Rais Nixon wa wakati huo nchini China mwaka 1972.

David Firestein Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya George H. W. Bush anayehusika na Uhusiano kati ya Marekani na China, ameiambia hafla hiyo kwamba kujenga uelewa wa China nchini Marekani ni jambo linalohitajika sana leo.

"Kwa hivyo, tunajaribu kukuza moyo wa huo wa ushirikiano" na mazungumzo, kujenga mazingira ya kiujenzi kwa diplomasia na ushirikishwaji, na kutetea sera za wastani zenye busara ambazo ni nzuri kwa Marekani, China, uhusiano wa pande mbili na dunia," amesema Firestein katika mahojiano na Shirika la Habari la China, Xinhua pembezoni mwa hafla hiyo.

"Tunachojaribu kufanya ni kusaidia kujenga uhusiano imara zaidi kati ya Marekani na China, kwa sababu tunaamini hilo ni muhimu sana," amesema Firestein.

Mabadilishano ya kati ya watu na watu ya China na Marekani yameshuhudia upigaji hatua wenye kutia moyo kutokana na dhamira kutoka pande zote mbili.

Wamarekani vijana zaidi ya 50,000 wametembelea China kupitia programu za kubadilishana na masomo chini ya mpango wa miaka mitano wa China, na kufikia lengo hilo miaka miwili na nusu kabla ya muda uliopangwa.

"Naipongeza serikali ya China kwa kufanya hivyo. Nadhani Marekani inahitaji kufanya zaidi, na natumai tutaona zaidi," Firestein amesema.

Akihutubia hadhira katika hafla hiyo, Balozi wa China nchini Marekani Xie Feng amesema kwamba Rais wa China Xi Jinping na Rais wa Marekani Donald Trump hivi karibuni walifanya mkutano wenye mafanikio mjini Beijing, ambapo pande hizo mbili zilikubaliana juu ya maono mapya ya uhusiano wa kiujenzi wa kati ya China na Marekani wenye utulivu wa kimkakati.

Amesisitiza kwamba kadri China na Marekani zinavyofika tena katika njia panda za kihistoria, pande hizo mbili zinahitaji zaidi kuliko hapo awali kutafuta msingi wa pamoja ili kusonga mbele pamoja.

"Katika muktadha huu, mabadilishano ya kati ya watu na watu na ya kitamaduni yamekuwa muhimu zaidi," amesema Xie.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha