Lugha Nyingine
Viwanda vya kahawa vyastawi katika Mji wa Jiangmen, Guangdong, China (2)
![]() |
| Jamaa akikata matawi na majani ya miti ya kahawa, huko Jiangmen, Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, Mei 25, 2026.(Xinhua/Deng Hua) |
Mji wa Jiangmen katika Mkoa wa Guangdong, kusini mwa China, mji maarufu wa makazi ya Wachina wanaorejea kutoka ng'ambo, umejenga viwanda vya aina yake ya kahawa kuanzia hatua za mwanzo kabisa.
Kwa kutumia mitandao yake duniani, mji huo umejenga mnyororo kamili wa kiviwanda, unaojumuisha mambo ya kuanzia uuzaji na ukaangaji wa kisasa wa maharage ya kahawa ya kijani hadi uzalishaji wa bidhaa, huku thamani ya mapato ya mwaka ikizidi yuan bilioni 3 (dola za Marekani takriban milioni 443).
Shukrani kwa uhusiano wake mkubwa na Wachina wa ng'ambo, mji huo wa Jiangmen ulikuwa kituo cha mapema kabisa kwa ajili ya ukaangaji kahawa nchini China. Leo hii, mji huo unaagiza aina zaidi ya 300 za maharage ya kahawa ya kijani ya hali ya juu kutoka nchi zinazozalisha kwa wingi kama vile Brazil, Ethiopia na Colombia. Na sasa ni nyumbani kwa jumla ya viwanda 21 vya wakaangaji vilivyoidhinishwa vyenye uwezo wa mwaka unaozidi tani 10,000.
Zaidi ya maharage, mji huo wa Jiangmen una kampuni zaidi ya 350 za ndani zinazozalisha zana na vipuri vya kahawa, unasambaza asilimia takriban 40 ya vifaa vya kahawa vya chuma kisicho shika kutu vya China na unazalisha mashine moja kati ya kila mashine tano za kahawa zinazouzwa nje kutoka China.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




