Sera za msamaha wa visa zachochea ongezeko la 35.3% katika utalii wa wageni wanaoingia Beijing

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2026
Sera za msamaha wa visa zachochea ongezeko la 35.3% katika utalii wa wageni wanaoingia Beijing
Watalii wa kigeni wakitembelea Eneo la Hekalu la Mbinguni (Temple of Heaven), Beijing, mji mkuu wa China, Mei 12, 2026. (Xinhua/Ju Huanzong)

Mji wa Beijing wa China ulipokea watalii jumla ya milioni 2.667 wanaoingia kutoka nje ya nchi katika miezi mitano ya kwanza ya mwaka huu, ongezeko la asilimia 35.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana, hali ambayo inaonyesha umaarufu unaozidi kuongezeka wa "Kusafiri Kutalii China."

Hadi kufikia Mei 11, idadi ya raia wa kigeni wa kutoka na kuingia katika bandari za Beijing ilikuwa imezidi milioni 2.55, ikichukua asilimia 32 ya jumla ya idadi yote ya abiria waingiao na watokao na kuonesha ukuaji wa asilimia 33.6 kutoka idadi ya mwaka jana.

Hadi kufikia tarehe hiyo hiyo, wasafiri wa kigeni takriban 957,000 waliowasili katika bandari za Beijing walikuwa wameingia chini ya sera za msamaha wa visa au ya vibali vya kuingia kwa muda, ikichukua asilimia 70.8 ya uingiaji wote wa wageni. Safari nyingi za wasafiri wanaoingia ni kwa madhumuni ya utalii, biashara, na kutembelea jamaa na marafiki.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha