Watoto wa vijijini wakimbilia ndoto za mpira wa miguu katika shule ya msingi, Anhui, China (2)

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 03, 2026
Watoto wa vijijini wakimbilia ndoto za mpira wa miguu katika shule ya msingi, Anhui, China
Watoto wakihudhuria kipindi cha mafunzo ya mpira wa miguu kwenye Shule ya Msingi ya Huikou katika Wilaya ya Susong ya Anqing, Mkoa wa Anhui, mashariki mwa China, Mei 26, 2026. (Xinhua/Du Yu)

Mji mdogo wa Huikou katika Wilaya ya Susong ya Anqing, Mkoa wa Anhui mashariki mwa China, uliopo kwenye mpaka unaounganisha mikoa ya Anhui, Hubei na Jiangxi, ni mji mdogo wa kwanza kando ya Mto Changjiang wakati ukitiririka kuingia mkoa huo wa Anhui.

Kinachoenea sambamba na mji huo mdogo ni ukingo wa Tongma, kizuizi cha mafuriko kinacholinda ardhi kando ya mto. Kando tu ya ukingo huo kuna Shule ya Msingi ya Huikou, ambapo uwanja wa mpira wa miguu wa wachezaji watano kwa kila upande umekuwa chimbuko la ndoto za mpira wa miguu za watoto wa vijijini.

Wachezaji zaidi ya 70 wa timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo huanza mazoezi yao ya asubuhi saa 1:30 asubuhi kila siku ya masomo. Hufanya mazoezi ya kupiga pasi fupi, kupiga shuti, kukimbia kwa kasi na mazoezi ya kujenga uimara wa mwili kwa saa moja.

Bidii yao endelevu imeipa timu ya mpira wa miguu ya shule hiyo heshima katika mashindano ya mpira wa miguu ya ngazi ya mji na mkoa, ikifikia upigaji hatua thabiti na mafanikio mapya katika maendeleo ya mpira wa miguu wa kampasi ya shule.

Mei Shisheng, kocha wa kudumu wa shule hiyo, amejitolea katika elimu ya vijijini tangu alipohitimu kutoka Chuo Kikuu cha Michezo cha Shanghai mwaka 2015. Kwake yeye mpira wa miguu ni zaidi ya tuzo na nafasi.

"Namna wanavyokumbatiana na kushangilia pamoja baada ya kufunga goli katika mechi za mashindano ya kati ya madarasa ni safi na inayogusa moyo. Nyakati hizi zinapita mchezo wenyewe," Mei amesema.

Uzoefu wa kupigana bega kwa bega uwanjani hukuza ustadi wa wachezaji hawa wachanga, na kuwajengea sifa za ushujaa, ustahimilivu, na kufanya kazi kama timu.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha