Wataalamu wa matibabu wa China na IFRC wajadiliana kuhusu hatua za kukabiliana na Ebola nchini DRC

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 10, 2026

Wajumbe wa timu ya wataalamu wa matibabu ya China na  wajumbe wa Shirikisho la Kimataifa la  Chama cha Msalaba Mwekundu na Chama cha Hilali Nyekundu (IFRC) wakijadili kuhusu hatua za kukabiliana na Ebola mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Juni 9, 2026. (Xinhua)

KINSHASA - Wajumbe wa timu ya wataalamu wa matibabu ya China wamekutana na wajumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Chama cha Msalaba Mwekundu na Chama cha Hilali Nyekundu (IFRC) huko Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) jana Jumanne, ambapo walijadili hali ya janga la Ebola, mahitaji ya kuzuia na kudhibiti, na maeneo ya kuweza kushirikiana.

Lu Ming, mkuu wa timu hiyo ya China, ameeleza nia ya kuimarisha ushirikiano na mamlaka za afya, taasisi za matibabu, mashirika ya kudhibiti ugonjwa nchini DRC, pamoja na washirika wa kimataifa ikiwemo IFRC.

Amesema kwamba timu hiyo itafanya juhudi za kuhamamishwa mahitaji halisi haraka iwezekanavyo katika kazi za kuzuia, kudhibiti, na usimamizi wa wagonjwa, na kutoa uungaji mkono katika kuchambua hali ya maambukizi ya virusi, kutibu wagonjwa, upimaji wa maabara, na mafunzo ya kuzuia na kudhibiti, ili kudhibiti maambukizi mapema iwezekanavyo.

Sonia Maraisse, meneja wa operesheni wa IFRC mjini Kinshasa, ameishukuru serikali ya China kwa kutuma timu hiyo ya wataalamu wa matibabu, akisema kwamba IFRC iko tayari kuimarisha mawasiliano na uratibu na upande wa China.

Amesema IFRC inakaribisha uungaji mkono huo ambao timu ya wataalamu wa China inaweza kutoa katika mafunzo ya kuzuia maambukizi, hasa mafunzo na uungaji mkono mahsusi katika sehemu za wakazi mashinani, ili kusaidia kuongeza uwezo wa watu wa jamii wa kugundua, kuzuia, na kukabiliana na maambukizi ya virusi vya ugonjwa. Timu hiyo ya wataalamu watano ya China ilifika Kinshasa Juni 2 kwa jukumu la miezi mitatu nchini DRC ili kuunga mkono mapambano dhidi ya janga la Ebola.

Shirika la Afya Duniani lilitangaza Mei 17 kwamba janga hilo la Ebola ni dharura ya afya ya umma inayohitaji umakini na ufuatiliaji wa kimataifa. Juni 1, Kamati ya Kitaifa ya Afya ya China ilitangaza kupeleka timu hiyo ya matibabu ya ngazi ya juu kwenda kuiunga mkono DRC katika mapambano yake dhidi ya Ebola.

Wajumbe wa timu ya wataalamu wa matibabu wa China na wajumbe wa Shirikisho la Kimataifa la Chama cha Msalaba Mwekundu na Chama cha Hilali Nyekundu (IFRC) wakijadili kuhusu hatua za kukabiliana na Ebola mjini Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Juni 9, 2026. (Xinhua)

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha