Lugha Nyingine
China yatoa wito kwa mataifa ya Afrika ya Kati kusukuma mbele mchakato jumuishi wa kisiasa
Naibu mjumbe wa kudumu katika Umoja wa Mataifa Balozi Sun Lei, Juni 9 kwenye mkutano wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya eneo la Afrika ya Kati alitoa wito kwa mataifa ya eneo hilo kusukuma mbele mchakato jumuishi wa kisasa na kulinda utulivu wa kikanda.
Balozi Sun amesema China inaunga mkono serikali za nchi mbalimbali za Afrika ya Kati kuendelea kusikiliza sauti za wananchi, kuendeleza mazungumzo shirikishi ya kisiasa na ujenzi wa utaratibu, na kuendelea kuimarisha umoja wa kitaifa na ufanisi wa kiutawala. Amesema, jamii ya kimataifa inapaswa kuheshimu kikamilifu mamlaka na uongozi wa nchi za kikanda, kuunga mkono mataifa ya eneo hilo kuendeleza mchakato wa amani na siasa kupitia mazungumzo na majadiliano, na kulinda mshikamano wa ndani na utulivu wa kikanda. Amebainisha kuwa, China inaunga mkono ofisi ya Umoja wa Mataifa katika eneo la Afrika ya Kati na mashirika ya kikanda kuongeza uratibu, na kukabiliana kwa pamoja na changamoto za kiusalama ikiwemo ugaidi na uhalifu wa kupangwa wa kuvuka mpaka, huku jumuiya ya kimataifa ikitakiwa kuzisaidia nchi za eneo hilo kuongeza uwezo wa kupambana na ugaidi na kudhibiti mipaka.
Balozi Sun amesisitiza kuwa, China inaunga mkono kithabiti masuala ya Afrika yatatuliwe na nchi za Afrika kwa njia za kiafrika, na inapenda kufanya juhudi pamoja na jumuiya ya kimataifa katika kuzisaidia nchi za eneo hilo kufuata njia mpya ya kujiendeleza kwa kujitegemea, na kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ajili ya kutimiza amani na ustawi wa kudumu katika eneo la Afrika ya Kati.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



