Lugha Nyingine
China yatoa mpango wa miaka mitatu wa kuhimiza mafungamano ya AI na sekta ya upashanaji wa habari na mawasiliano ya habari

Mfanyakazi akielezea matumizi ya nguvu ya mahesabu ya kompyuta kwenye kampuni ya sayansi na teknolojia ya upashanaji habari, huko Hohhot, Mkoa wa Mongolia ya Ndani, Kaskazini mwa China, Juni 4, 2026. (Xinhua/Li Zhipeng)
BEIJING – Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya Upashanaji Habari ya China imetoa mpango wa miaka mitatu jana Jumatano ili kuharakisha mafungamano ya teknolojia ya AI na sekta ya upashanaji habari na mawasiliano ya habari ya China, ikiweka malengo ya kuifanya mitandao mingi inayoweza kujiendesha yenyewe, upatikanaji mpana zaidi wa nguvu ya mahesabu ya kompyuta kwa muda wa chini na matumizi yaliyopanuliwa ya AI ifikapo mwaka 2028.
Mwongozo huo wa utekelezaji unaohusisha kazi za mwaka 2026 hadi mwaka 2028, unalenga mitandao ya kupashana habari na mawasiliano ya habari kufikia kipindi cha mwanzo cha kujiendesha kwa teknolojia ya AI kwenye kiwango cha juu ifikapo mwaka 2028.
Pia mpango huo unatoa matakwa ya kufikia matumizi zaidi ya 30 yenye thamani kubwa, matumizi kadhaa katika mazingira ya kawaida na mawakala maalum wa AI, vilevile usambazaji huduma wa angalau asilimia 75 kuhusu ufikiaji wa nguvu ya kompyuta kwa muda mfupi zaidi wa milisekunde-moja katika maeneo ya miji mikubwa.
Wizara hiyo imesema teknolojia za AI ziko katika kipindi cha kubadilika kila mara na kupata mafanikio mapya kwa haraka, wakati huohuo mafungamano ya kina ya AI na upashanaji habari na mawasiliano ya habari bado ni kazi ngumu yenye utatanishi, tena ni ya kimfumo, kutokana na changamoto katika kujipatia mafanikio katika teknolojia muhimu, njia za mafungamano na uvumbuzi wa mifumo ya biashara.
Hadi kufikia 2030, China inalenga kupata mafanikio makubwa kwenye teknolojia za maeneo muhimu kwa ajili ya mafungamano ya AI na mitandao ya kupashana habari na mawasiliano ya habari, kuongeza zaidi uwezo wa kuhisi kwa ujumla, mawasiliano ya habari, mahesabu ya kompyuta na uwezo wa huduma za AI, na kujenga mfumo kamili wa ushirikiano kati ya uvumbuzi na hali ya ikolojia ya viwanda.
Wizara hiyo imeweka majukumu 17 katika maeneo manne, ambayo ni kupanda ngazi mpya ya AI katika kazi za kupashana habari na mawasiliano ya habari, kuimarisha msingi wa maendeleo ya AI, kuhimiza mafungamano ya matumizi na kuboresha usimamizi wa sekta.
Pia inatoa wito wa kufanya utafiti katika usanifu mpya wa mtandao unaoendeshwa kwa teknolojia ya AI, upigaji hatua wa pamoja kati ya mifumo mikubwa na midogo, ushirikiano kati ya mifumo mbalimbali ya AI, na mawasiliano ya habari ya AI, kuharakisha ujenzi wa njia kuu za nguvu za mahesabu ya kompyuta na kupanga vizuri rasilimali za mtandao.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



