Lugha Nyingine
Wazalishaji bidhaa wa China wang'aa kwenye maonyesho ya miundombinu ya Afrika Kusini

Watu wakizungumza kwenye Maonyesho ya Miundombinu ya Afrika Kusini jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 10, 2026. (Xinhua/Chen Wei)
JOHANNESBURG –Maendeleo ya wazalishaji bidhaa wa China umevutia ufuatiliaji mkubwa kwenye Maonyesho ya Miundombinu ya Afrika Kusini yaliyofanyika kuanzia Jumanne hadi Alhamisi jijini Johannesburg, jiji kubwa zaidi la Afrika Kusini.
Maonyesho hayo yaliyofanyika sambamba na Big 5 Construct South Africa na Transport Evolution Africa, yalikuwa ni sehemu ya jukwaa la viwanda jumuishi lililohusu mambo kama vile miundombinu, usafiri na ujenzi, likiwa na waonyeshaji bidhaa kutoka nchi na maeneo zaidi ya 25.
Kampuni karibu 120 za China zimeshiriki katika maonyesho hayo, zikionyesha bidhaa na huduma zinazohusiana na mashine za ujenzi, vifaa vya bomba na maji, nyenzo za barabarani, nyenzo za ujenzi na vifaa, na usafirishaji wa kutumia teknolojia zenye AI.
Waonyeshaji bidhaa wa China wanaona nguvu bora katika soko la Afrika Kusini, ambapo ukuaji wa mahitaji ya miundombinu na kuongezeka kwa matarajio ya wateja kwa ufanisi wa vifaa, gharama za uendeshaji, na uungaji mkono wa baada ya kununuliwa vifaa husika vinatengeneza nafasi kwa bidhaa na suluhu zaidi zilizojanibishwa.
Kwa mfano, katika banda la Kundi la SANY, mzalishaji mkuu wa vifaa vizito wa China, malori ya kubeba mizigo mizito yenye kutumia umeme, forklifti za umeme, na telehandlers vilikuwa miongoni mwa mambo yaliyokuwa yakifuatiliwa zaidi. Kampuni hiyo imeonyesha upigaji hatua wake katika kuzifanya mashine za ujenzi kuwa zenye kutumia umeme, kwa kuweka mkazo katika ujenzi, usafirishaji, na uhifadhi wa kwenye maghala.
Guan Di, international marketing manager of SANY Marine Heavy Industry Co., Ltd., said South Africa has a solid industrial foundation and a relatively mature transport system, giving the market strong potential.
Guan Di, meneja masoko wa kimataifa wa SANY Marine Heavy Industry, amesema Afrika Kusini ina msingi imara wa kiviwanda na mfumo wa usafiri uliokomoo kwa kiasi kikubwa, hali ambayo inalipa soko nguvu bora thabiti.
"Gharama kubwa za mafuta katika nchi hii pia zimefanya vifaa vya umeme kuwa vyenye kupendelewa zaidi na wateja wenyeji," Guan amesema.
Kadri wateja wanavyozingatia zaidi uhakika wa vifaa, gharama za uendeshaji na huduma za baada ya kununua vifaa husika; ubora wa bidhaa, mitandao ya huduma, na uwezo wa kutoa bidhaa mahsusi vinazidi kuwa muhimu kwa kampuni za China zinazopanuka katika masoko ya Afrika.
Mbali na kampuni kubwa za mashine za ujenzi, kampuni binafsi za China katika sekta zinazohusiana na miundombinu pia zinaitumia Afrika Kusini kama kituo muhimu cha kuzidisha uwepo wao barani Afrika.
Jin Dandan, meneja mkuu wa kampuni ya Shanxi Jinbiao Photoelectric Technology amesema kampuni yake imehudhuria maonyesho hayo nchini Afrika Kusini kwa mara ya kwanza na inapanga kupanua zaidi katika soko la Afrika mwaka huu.
Mameetse Masemola, mkuu wa Miundombinu Afrika Kusini, ameliambia Shirika la Habari la China, Xinhua kwamba Afrika Kusini inatarajia kutumia uzoefu wa China katika maendeleo ya miundombinu.
"China ina teknolojia za kisasa na mbinu mpya kwa ajili ya ujenzi, na inaongoza dunia katika miundombinu," amesema.

Watu wakitembelea Maonyesho ya Miundombinu ya Afrika Kusini jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 10, 2026. (Xinhua/Chen Wei)

Watu wakizungumza kwenye Maonyesho ya Miundombinu ya Afrika Kusini jijini Johannesburg, Afrika Kusini, Juni 10, 2026. (Xinhua/Chen Wei)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



