China yapata maendeleo makubwa katika kunyanyua haki za binadamu

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 12, 2026

Picha hii iliyopigwa Juni 11, 2026 ikionyesha hali ya ufunguzi wa Jukwaa la 2026 la Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Cai Yang)

Picha hii iliyopigwa Juni 11, 2026 ikionyesha hali ya ufunguzi wa Jukwaa la 2026 la Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Cai Yang)

BEIJING - China imetoa mpango utendaji wa kitaifa wa kunyanyua haki za binadamu katika miaka mitano ijayo kwenye Jukwaa la mwaka 2026 linaloendelea kuhusu Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani, ambapo wahudhuriaji kutoka ndani na nje ya nchi wamesifu maendeleo ya China katika nyanja hiyo. 

Mpango utendaji wa Kitaifa wa Haki za Binadamu wa China (2026-2030) unalenga kuhakikisha nafasi kuu ya watu inaheshimiwa na maslahi ya kimsingi ya watu yanalindwa.

Pia mpango huo utahimiza usawa na haki kwenye jamii, na kuhakikisha matunda ya ujenzi wa mambo ya kisasa yananufaisha watu wote kwa usawa.

Mpango utendaji huo unaweka malengo na majukumu makuu ya miaka mitano ijayo, ikiwemo kuhimiza uhakikishaji wa pande zote wa haki za kiuchumi, kijamii na kitamaduni kwa kupitia maendeleo yenye sifa bora, kukamilisha mifumo ya kulinda haki za raia katika mambo ya kiraia na kisiasa, na kuimarisha ulinzi wa haki za mazingira.

Kwa mujibu wa mpango utendaji huo, China pia itahakikisha ulinzi sawa wa haki na maslahi ya makundi yote, kuongoza maendeleo mazuri ya nyanja zinazoibuka za haki za binadamu, kuendelea kuongeza uelewa wa haki za binadamu, na kuhimiza usimamizi wa haki za binadamu duniani.

Jukwaa la mwaka 2026 la Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani limeanza Beijing jana Alhamisi, likifuatilia zaidi kujipatia maendeleo kwa pamoja na kunufaika pamoja na haki za binadamu.

Wageni wanaohudhuria jukwaa hilo wamesema kwa kauli moja kwamba kadiri China inavyosukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa, imeendelea kuimarisha uhakikisho wa haki za binadamu na kupata maendeleo ya kihistoria katika kuhimiza haki za binadamu.

Picha hii iliyopigwa Juni 11, 2026 ikionyesha wahudhuriaji kwenye ufunguzi wa Jukwaa la 2026 la Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani, uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Cai Yang)

Picha hii iliyopigwa Juni 11, 2026 ikionyesha wahudhuriaji kwenye ufunguzi wa Jukwaa la 2026 la Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani, uliofanyika Beijing, mji mkuu wa China. (Xinhua/Cai Yang)

Grigory Lukiyantsev, mwakilishi maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia anayeshughulikia Haki za Binadamu, Demokrasia na Utawala wa Kisheria , amesema kwamba China imepata maendeleo makubwa katika kulinda haki za binadamu.

"Kwa kweli ni mfano ambao wengine wanaweza kujifunza," Lukiyantsev amesema.

Ripoti ya hivi karibuni iliyotathmini utekelezaji wa Mpango Utendaji wa Nne wa Kitaifa wa Haki za Binadamu wa China (2021-2025) imeonesha kuwa China imeimarisha ulinzi wa haki za binadamu katika pande mbalimbali na kukamilisha majukumu 181 yaliyowekwa katika mpango utendaji huo wa miaka mitano.

Jukwaa hilo la siku mbili lina kaulimbiu isemayo "Kujipatia Maendeleo kwa Pamoja, Kunufaika Pamoja na Haki za Binadamu: Maadhimisho ya Miaka 40 tangu Kupitishwa kwa Azimio la Haki ya Maendeleo na Matarajio Mapya kwa Usimamizi wa Haki za Binadamu Duniani." Jukwaa hilo limevutia washiriki zaidi ya 400 kutoka nchi zaidi ya 100 na mashirika ya kimataifa, ukiwemo Umoja wa Mataifa.

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha