Lugha Nyingine
Wataalamu watoa wito wa kuzidisha ushirikiano wa China-Afrika katika nishati wakati wa mgogoro wa Mashariki ya Kati

Jiang Feng, mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika (AU), akitoa hotuba kwenye Jukwaa la Nishati la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika 2026, Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Juni 11, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
ADDIS ABABA - Maofisa na wataalamu kutoka China na nchi za Afrika wametoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa pande mbili katika maendeleo ya nishati ili kuhakikisha utoaji wa nishati unaendelea, ulio wa bei nafuu na wa kuaminika, na pia kwa kukabiliana na hali wasiwasi duniani, hasa mivurugiko katika usafirishaji wa mafuta unaosababishwa na mgogoro katika Mashariki ya Kati.
Wito huo umetolewa jana Alhamisi kwenye Jukwaa la Nishati la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika 2026, lililofanyika Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, chini ya kaulimbiu ya "Kuimarisha Diplomasia ya Nishati ya China na Afrika katika Dunia Yenye Misukosuko."
Akizungumza kwenye jukwaa hilo, Jiang Feng, mkuu wa Ujumbe wa China katika Umoja wa Afrika (AU), amesema China na Afrika zinahitaji kujenga uhusiano wa wenzi wa ushirikiano wa nishati ulio wa kunufaishana na kupata maendeleo kwa pamoja ili kuhakikisha utoaji endelevu wa nishati.
"Katika kukabiliana na mahitaji ya nishati ya dharura ya Afrika, ushirikiano wa nishati kati ya China na Afrika unapaswa kuweka mkazo katika kuendeleza rasilimali za nishati mbadala, kuingiza teknolojia za kutoa kaboni chache, kuunga mkono Afrika kuongeza uwezo wa kusafisha mafuta, na kujenga gridi imara za umeme ili kuhakikisha utoaji nishati wenye ufanisi kote barani," Jiang amesema.
Ameongeza kuwa China inapenda kuchangia uzoefu wake na kuisaidia Afrika kuhuisha maliasili zake nyingi za nishati wakati huohuo kuboresha upatikanaji wa nishati za kuaminika kwa njia ya kisasa.
Erastus Mwencha, naibu mwenyekiti wa zamani wa Kamisheni ya AU na mwenyekiti wa sasa wa Bodi ya Benki ya Equity Kenya, amesema China na Afrika zinapaswa kuendeleza uzalishaji wa nishati safi na kupunguza hali ya kutegemea kwa kupindukia kiasi juu ya nishati ya visukuku, na wakati huo huo kutumia mifumo iliyopo ya ushirikiano.
Amesema kuwa mfumo wa ushirikiano wa nishati uliopitishwa kwenye Mkutano wa Beijing wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, pamoja na mpango utendaji wake, vinatoa msingi imara wa taratibu kwa ajili ya kukabiliana na msukosuko wa sasa wa nishati duniani.
Huku akieleza kwamba kufungwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz katika Mashariki ya Kati kumezifanya nchi za Afrika zikabiliwe na changamoto kali zaidi za usalama wa nishati duniani, Mwencha amesema ushirikiano uliopo sasa wa nishati kati ya China na Afrika unaweza kutumika kama chombo cha kuhimiza juhudi za kupunguza hatari ya misukosuko ya sasa na ya siku za baadaye ya nishati duniani.
Jukwaa la Nishati la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika 2026, lililoandaliwa na Taasisi ya Sera ya Afrika, limevutia wataalamu na wasomi karibu 100 kutoka China na Afrika.

Erastus Mwencha, naibu mwenyekiti wa zamani wa Kamisheni ya AU na mwenyekiti wa sasa wa Bodi ya Benki ya Equity Kenya, akitoa hotuba kwenye Jukwaa la Nishati la Jumuiya za Washauri Bingwa za China na Afrika 2026, Addis Ababa, mji mkuu wa Ethiopia, Juni 11, 2026. (Picha na Michael Tewelde/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



