Lugha Nyingine
China yaendelea na juhudi kubwa za kuwa jirani na mshirika mzuri wa kuaminiana na kuunga mkono kushughulikia uhusiano na Mongolia

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mongolia Batmunkh Battsetseg kwa pamoja wakikutana na waandishi wa habari mjini Ulan Bator, Mongolia, Juni 13, 2026. (Xinhua/Bolortsetseg)
ULAN BATOR - Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), amesema kwamba mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mongolia Batmunkh Battsetseg yamepata maoni ya pamoja kuhusu masuala mengi juu ya uhusiano wa pande mbili na ushirikiano wa kikanda.
Akizungumza kwenye mkutano wa pamoja na waandishi wa habari Jumamosi mjini Ulan Bator, Mongolia, Wang alisema pande zote mbili zimekubaliana kwamba, katika mazingira ya kimataifa yenye misukosuko na changamoto zinazoikabili dunia na kuzidi kuwa utatanishi, China na Mongolia zinapaswa kusimama pamoja kwa kukabiliana na taabu na kusaidiana na kuendelea kufanya juhudi za kujenga jumuiya ya China na Mongolia yenye mustakabali wa pamoja iliyo ya kuishi pamoja kwa amani, kuungana mkono, na kufanya ushirikiano wa kunufaishana na kutafuta maendeleo kwa pamoja.
Amesema, nchi hizo mbili zimesisitiza kuwa, kila upande unaheshima msimamo wa upande mwingine kuhusu uhuru wa kujitawala, mamlaka ya nchi, na ukamilifu wa ardhi, na kuahidi kuheshimu maslahi ya kimsingi, mambo makubwa yanayofuatiliwa, na njia ya kujiendeleza iliyochaguliwa na upande mwingine.
Wang ameeleza kuwa China inasifu Mongolia kufuata kanuni ya kuwepo kwa China moja, kupinga vitendo vya aina yoyote vya kuifanya "Taiwan ijitenge," na kuunga mkono misimamo ya China juu ya masuala ya Taiwan, Hong Kong, Xinjiang, na Xizang. Wang amesema, China siku zote ni mshirika anayeaminika kwa Mongolia na itaendelea kutoa uungaji mkono wakati wowote Mongolia itakapokuwa na uhitaji zaidi.
Wang amesema kuwa ujenzi wa mambo ya kisasa ni lengo la pamoja kwa nchi zote mbili. Kwa kutazama siku za baadaye, pande hizo mbili zitahimiza kuhusisha Pendekezo la Ukanda Mmoja, Njia Moja na mkakati wa maendeleo ya malisho makubwa wa Mongolia, kuzidisha mabadilishano juu ya uzoefu wa utawala, kutafuta fursa za kufanya ushirikiano katika sekta zinazoibukia, na kwa pamoja kufuata njia za ujenzi wa mambo ya kisasa zinazolingana na hali halisi ya kila nchi kati yao.
Amesema China na Mongolia zote ni nguvu za kiujenzi kwa amani, utulivu, na maendeleo ya dunia, na nchi hizo mbili zina nia ya kuimarisha uratibu katika mambo ya kikanda na kimataifa na kufanya juhudi za pamoja ili kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.
In addition, both countries agreed to enhance coordination within multilateral frameworks such as the Shanghai Cooperation Organization and the Asia-Pacific Economic Cooperation to jointly promote regional stability, development, and cooperation.
Zaidi ya hayo, alisema nchi zote mbili zimekubaliana kuongeza uratibu ndani ya mifumo ya pande nyingi kama vile Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na Ushirikiano wa Kiuchumi wa Asia-Pasifiki ili kuhimiza kwa pamoja utulivu, maendeleo, na ushirikiano wa kikanda.

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi, ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, na Waziri wa Mambo ya Nje wa Mongolia Batmunkh Battsetseg (hayupo kwenye picha) wakikutana kwa pamoja na waandishi wa habari mjini Ulan Bator, Mongolia, Juni 13, 2026. (Xinhua/Bolortsetseg)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



