Makubaliano kati ya Marekani na Iran yafikiwa, Mlango-Bahari wa Hormuz kufunguliwa tena

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Juni 15, 2026

Picha hii iliyopigwa Juni 7, 2026 ikionyesha ishara ya kuwataka watu kusimama na jengo la Bunge la Marekani, The Capitol, kwa nyuma, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)

Picha hii iliyopigwa Juni 7, 2026 ikionyesha ishara ya kuwataka watu kusimama na jengo la Bunge la Marekani, The Capitol, kwa nyuma, Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)

WASHINGTON - Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba makubaliano ya amani kati ya Marekani na Iran "sasa yamekamilika" na kwamba Mlango-Bahari wa Hormuz utafunguliwa tena baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo baadaye Ijumaa wiki hii.

"Makubalino na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sasa yamekamilika," Trump ameandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social jana Jumapili. "Kwa hivyo ninaidhinisha kikamilifu kufunguliwa kwa Mlango-Bahari wa Hormuz bila tozo, na, wakati huo huo, ninaidhinisha kuondolewa mara moja kwa kizuizi cha Kikosi cha Majini cha Jeshi la Marekani."

"Meli za Dunia, washa injini zenu. Acha mafuta yatiririke!" amesema Trump.

Amesema katika ujumbe wake mwingine kwenye mtandao huo dakika chache baadaye kwamba mlango-bahari huo utafunguliwa tena baada ya kusainiwa kwa makubaliano hayo Ijumaa.

"Kwa kufunguliwa kwa Mlango-Bahari baada ya kusainiwa makubalino siku ya Ijumaa, kwa madhumuni ya kuondolewa kwa mabomu baharini, mafuta yatatiririka pande zote mbili tena kwa Kanda hiyo, na Dunia!" Trump amesema.

Muda mfupi kabla ya ujumbe huo wa Trump kuhusu makubaliano hayo, Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alisema kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa X kwamba hafla rasmi ya kusaini makubaliano hayo imepangwa kufanyika Juni 19 nchini Uswisi.

Makubaliano hayo yatasainiwa kielektroniki na yeye au na Makamu Rais JD Vance ana kwa ana, Trump ameliambia jarida la The Wall Street katika mahojiano.

Trump ameliambia Jarida hilo kwamba makubaliano hayo yatajumuisha ahadi kutoka Iran ya kutopata silaha za nyuklia na kufunguliwa tena mara moja kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.

Pia alisema kwamba hakuna udharura wa kutoa vitu vya nyuklia kutoka Iran, akisema "hakuna haraka."

Kutakuwa na ukaguzi mkali wa nyuklia kwa Iran, Trump amesema, bila kueleza mahsusi ni kwa namna gani utafanyika.

Trump ameongeza kuwa chini ya makubaliano hayo, Iran haitapewa pesa taslimu lakini vikwazo vinaweza kuondolewa.

"Tutaona jinsi watakavyotenda," amesema.

Trump pia amedai Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anaunga mkono makubaliano hayo.

Kituo cha televisheni cha IRIB cha Iran, kinachoendeshwa na serikali, kikimrejelea Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayehusika na Sheria na Masuala ya Kimataifa, Kazem Gharibabadi, kimesema kuingia kwa Iran katika kipindi cha siku 60 cha mazungumzo na Marekani juu ya mpango wake wa nyuklia na kuondolewa kwa vikwazo kutategemea Marekani kutimiza ahadi zake za awali, ambazo zitathibitishwa na Tehran kuanzia sasa hadi kufikia siku ya hafla ya utiaji saini.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha