Lugha Nyingine
Barabara ya kitaifa iliyojengwa na kampuni ya China yataboresha hali ya usafiri kusini mashariki mwa Madagascar

Picha hii iliyopigwa Juni 13, 2026 ikionyesha sehemu ya ujenzi wa kipindi cha kwanza wa Barabara ya Kitaifa No, 12 iliyojengwa na kampuni ya China, huko Taolagnaro, Madagascar. (Xinhua/Chen Shaohua)
TAOLAGNARO, Madagascar – Hafla ya kuzinduliwa kwa sehemu ya ujenzi wa kipindi cha kwanza wa Barabara ya Kitaifa No. 12 iliyojengwa na kampuni ya China imefanyika Jumamosi huko Taolagnaro, mji wa pwani ulioko kusini mashariki mwa Madagascar, ambapo Rais wa nchi hiyo Michael Randrianirina na Waziri Mkuu Mamitiana Rajaonarison wameshiriki kwenye hafla hiyo.
Sehemu ya barabara ya ujenzi wa kipindi cha kwanza wa Barabara ya Kitaifa No. 12 iliyojengwa na Kampuni ya Kundi la Shirika la 18 la Reli la China iko katika mkoa wa Anosy kusini mashariki mwa nchi hiyo. Ina urefu wa kilomita takriban 45 na ikiwemo pamoja na madaraja matano. Baada ya kukamilika na kuanza kutumika rasmi, itakuwa njia kuu ya usafiri kusini mashariki mwa Madagascar.
Kwenye hafla hiyo ya kukamilika kwa ujenzi wa sehemu hiyo ya barabara, Randrianirina alisema kwamba kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo kuna umuhimu mkubwa kwa wakazi wanaoishi kando za barabara hiyo, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wamesumbuliwa na hali mbaya ya usafiri.

Rais wa Madagascar Michael Randrianirina (wa kwanza kushoto) akitoa hotuba kwenye hafla ya kuzinduliwa rasmi kwa sehemu ya barabara ya ujenzi wa kipindi cha kwanza ya Barabara ya Kitaifa No. 12 iliyojengwa na kampuni ya China, Taolagnaro, Madagascar, Juni 13, 2026. (Xinhua/Chen Shaohua)
“Ingawa timu ya ujenzi ilikumbwa na matatizo mbalimbali wakati wa ujenzi, lakini imezishinda vizuizi hatua kwa hatua na kupata matokeo halisi,” aliongeza.
Rais huyo alipotoa hotuba pia aliwauliza wakazi wa huko kuhusu maoni yao ya kuridhika na ubora wa mradi huo, na kwa kauli moja walijibu kwamba "wameridhika".
Qiu Yuliang, naibu meneja mkuu wa Kampuni ya Kundi la Shirika la 18 la Reli la China alisema mradi huo ni sehemu muhimu ya mtandao wa barabara wa kitaifa wa Madagascar.
Alisema, kukamilika kwake kutaboresha kwa udhahiri hali ya mawasiliano ya barabara ya huko, kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa na kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa bidhaa za uvuvi kando za barabara, wakati huohuo kuchochea maendeleo ya sekta za uvuvi, madini, na utalii.
Hafla nyingine ya uzinduzi wa ujenzi wa kipindi cha pili wa mradi huo wa Barabara ya Kitaifa Nambari 12 inayojengwa na kampuni hiyo ya China pia ilifanyika siku hiyo hiyo.

Picha hii iliyopigwa Juni 13, 2026 ikionyesha sehemu ya barabara ya ya ujenzi wa kipindi cha kwanza ya Barabara ya Kitaifa No, 12 iliyojengwa na kampuni ya China, huko Taolagnaro, Madagascar. (Kundi la 18 la Shirika la Reli la China/kupitia Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



