Lugha Nyingine
Safari za kuvuka mpaka kupitia vituo vya Beijing, China zazidi milioni 10 hadi katikati ya Juni
![]() |
| Abiria wakipitia taratibu za ukaguzi wa mpakani kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Beijing, China Juni 15, 2026. (Xinhua/Li Xin) |
BEIJING – Kituo kikuu cha ukaguzi wa kutoka na kuingia Beijing kimetoa habari zikisema kuwa, safari za kuvuka mpaka kupitia vituo vya Mji wa Beijing, China zimezidi milioni 10 kwa jumla hadi jana Jumatatu, zikifikia ongezeko la asilimia 10.5 kuliko zile za kipindi kama hicho mwaka jana, na kufikia idadi hiyo kubwa kwa nusu mwezi mapema kuliko mwaka 2025.
Liu Yan wa kituo hicho amesema kuwa, kati ya wasafiri wote, safari za raia wa kigeni zilichukua asilimia zaidi ya 30, zikifikia zaidi ya milioni 3.4, na ni ongezeko la asilimia zaidi ya 30 kuliko zile za kipindi kama hicho mwaka jana.
“Kati ya wasafiri wote wa kigeni walioingia, zaidi ya milioni 1.25 waliingia China kupitia maingilio ya Beijing chini ya msamaha wa visa au sera za vibali vya muda vya kuingia,” Liu amesema, akiongeza, wengi wa wageni hao waliowasili ni watalii wa kutazama mandhari, wa kufanya mazungumzo ya kibiashana au wa kujumuika pamoja na familia.
Amesema wakazi wa China Bara walifanya safari milioni 6.033 za kuvuka mipaka kupitia vituo vya kutoka vya Beijing hadi kufikia sasa mwaka huu, huku Jamhuri ya Korea, Thailand na Singapore zikiwa sehemu zinazopendelewa zaidi kwa wasafari hao wa kwenda nje ya nchi.
Kwa sasa China inatekeleza hatua mfululizo za kurahisisha taratibu za kutoa visa, zikiwa ni pamoja na msamaha wa visa wa upande mmoja, kusameheana visa na sera za msamaha wa visa za kuingia China kusubiri ndege kwenda nchi nyingine kwa raia wa nchi mbalimbali.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




