Lugha Nyingine
Shehena ya kwanza ya China ya vitu vya msaada kwa waathirika wa tetemeko la ardhi yawasili Venezuela

Shehena ya kwanza ya vitu vya msaada wa dharura wa ubinadamu uliotolewa na serikali ya China kwa Venezuela ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Simon Bolivar wa Maiquetia, karibu na mji mkuu wa Venezuela, Caracas, Julai 6, 2026. (Picha na Marcos Salgado/Xinhua)
CARACAS - Shehena ya kwanza ya vitu vya msaada wa dharura wa ubinadamu uliotolewa na serikali ya China kwa Venezuela imewasili Jumatatu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Simon Bolivar wa Maiquetia, karibu na mji mkuu wa Venezuela, Caracas.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela Yvan Gil na Balozi wa China nchini Venezuela Lan Hu walipokea vitu hivyo katika uwanja wa ndege.
Gil akiwa kwa niaba ya watu wa Venezuela ameishukuru serikali ya China na viongozi wake kwa kutoa vitu hivyo vya msaada, akisema China imedumisha mawasiliano ya karibu na serikali ya Venezuela tangu matetemeko ya ardhi yalipotokea.
"Vitu hivyo vya msaada, vikiwemo mahema na jenereta, ni vyenye umuhimu mkubwa kwa watu waliopoteza nyumba zao katika janga hilo," Gil amesema, akiongeza kuwa msaada huo unaonyesha ushirikiano wa kimkakati wa hali zote wa kudumu kati ya nchi hizo mbili.
Gil amesema Wachina wa maeneo ya makazi nchini Venezuala na kampuni zinazowekezwa na China nchini Venezuela wametoa msaada mkubwa baada ya kutokea kwa matetemeko ya ardhi, wakishiriki kwenye kazi za uokoaji na kusaidia wakazi waliopoteza nyumba zao tangu mwanzo.
"Mengi ya msaada uliotolewa na hao Wachina yalikuwa ya kugusa moyo sana," amesema, akiongeza kuwa watu wa Venezuela wameona uungaji mkono huo na kwamba watu wa pande hizo mbili, wanaoishi katika ardhi moja, wamejenga urafiki mkubwa.
Usiku wa Juni 24, Venezuela ilikumbwa na matetemeko makali ya ardhi yenye nguvu zaidi yaliyotokea katika miaka zaidi ya mia moja iliyopita, ambapo matetemeko mawili ya ardhi yenye nguvu kubwa zaidi ya kipimo cha 7 yalitokea ndani ya dakika moja. Matetemeko hayo ya ardhi hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 3,342 na wengine 16,740 kujeruhiwa.

Shehena ya kwanza ya vitu vya msaada wa dharura wa ubinadamu uliotolewa na serikali ya China kwa Venezuela ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Simon Bolivar wa Maiquetia, karibu na mji mkuu wa Venezuela, Caracas, Julai 6, 2026. (Picha na Marcos Salgado/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



