Lugha Nyingine
Vifo kutokana na Ebola nchini DRC vyazidi 500 na maambukizi yanaendelea

Wafanyakazi wa matibabu wakivaa mavazi ya kujikinga kwenye kituo cha matibabu ya Ebola, Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 6, 2026. (Xinhua)
KINSHASA - Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa sasa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imezidi 500, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumapili na mamlaka za afya za nchi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, nchi hiyo imerekodi watu 1,561 waliothibitishwa kuwa na maambukizi, vikiwemo vifo 506. Jumla ya wagonjwa 254 wamepona, huku wagonjwa 628 waliothibitishwa kwa sasa wako katika karantini au hospitalini.
Mamlaka pia zimebainisha watu 354 wanaoshukiwa kwa ugonjwa huo, vikiwemo vifo 110.
Majaribio hayo ya matibabu yameanza kwenye kituo cha matibabu ya Ebola cha CME katika kanda ya afya ya Rwampara iliyoko Jimbo la Ituri, ambalo ni kiini cha mlipuko huo, kwa mujibu wa ripoti hiyo.

Wafanyakazi wa matibabu wakifanya kazi ya kuua vijidudu kwenye kituo cha matibabu ya Ebola, Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 6, 2026. (Xinhua)

Wafanyakazi wa matibabu wakifanya kazi ya kuua vijidudu kwenye kituo cha matibabu ya Ebola, Bunia, mji mkuu wa Jimbo la Ituri katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Julai 6, 2026. (Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



