Vikosi vya Kamandi ya Kati ya Marekani vyaanzisha mashambulizi makali dhidi ya Iran

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 08, 2026

WASHINGTON - Vikosi vya Marekani vilianzisha mashambulizi dhidi ya Iran jana Jumanne baada ya meli tatu za kibiashara zilizokuwa zikipita kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz kushambuliwa, Kamandi ya Kati ya Marekani imesema.

Vikosi vya Marekani "vimeanza kufanya mfululizo wa mashambulizi makali dhidi ya Iran ili kuifanya ilipe gharama kubwa kwa kulenga na kushambulia meli za kibiashara zinazoendeshwa na raia wasio na hatia kwenye njia ya maji ya kimataifa," kamandi hiyo imesema katika ujumbe wake kwenye mtandao wa X.

"Mashambulizi ya Marekani yanajibu mashambulizi ya Iran dhidi ya meli tatu za kibiashara zilizokuwa zikipitia kwenye Mlango-Bahari wa Hormuz," imesema kamandi hiyo.

Milipuko ilisikika karibu na Kisiwa cha Qeshm cha Iran na miji ya bandari ya Bandar Abbas na Sirik, kwa mujibu wa chombo cha habari cha serikali ya Iran Press TV.

Shirika la Uendeshaji wa Biashara za Baharini la Uingereza Jumanne liliripoti mashambulizi matatu tofauti yaliyolenga meli za mafuta zilizokuwa zikipita kwenye Mlango Bahari wa Hormuz, bila kuripotiwa majeruhi.

(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)

Picha