Lugha Nyingine
“China Imeweza Kufanikiwa, na Nchi Zingine Zinazoendelea Zinaweza Kufanikiwa Vilevile”
Kutimiza mambo ya kisasa imekuwa ni jitihada isiyokoma ya watu wa China tangu zama za karibuni, na pia ni matarajio ya pamoja ya watu wa mataifa yote duniani.
"China imeweza kufanikiwa, na nchi zingine zinazoendelea zinaweza kufanikiwa vilevile." "Tumedhamiria kithabiti kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, na kuwa na maono ya kuchangia fursa za maendeleo na dunia kupitia ufunguaji mlango wa kiwango cha juu, tutaingiza imani na nguvu katika ukuaji wa uchumi duniani kupitia maendeleo yetu wenyewe." Mapendekezo na kauli hizo muhimu zilizotolewa na Katibu Mkuu Xi Jinping zimejikita katika vitendo vilivyofanikiwa vya ujenzi wa mambo ya kisasa wa China, na zinadhihirisha dhamira na uwajibikaji wa China katika kushirikiana na nchi mbalimbali kwenye njia ya ujenzi wa mambo ya kisasa, kwa pamoja kusukuma mbele mambo ya kisasa duniani na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.
Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China ni mambo ya kisasa yenye sifa ya ustawi wa pamoja wa watu wote. Chini ya uongozi wa Katibu Mkuu Xi Jinping, China siku zote imelifanya jambo la kutimiza matarajio ya watu kwa maisha bora kuwa sehemu ya kuanzia na lengo kuu la jitihada zake za ujenzi wa mambo ya kisasa, ikisukuma mbele ustawi wa pamoja kwa hatua thabiti.
Muhtasari wa "Mpango wa 15 wa Miaka Mitano" unashikilia falsafa ya maendeleo yanayotilia maanani zaidi watu, ukiweka mpangilio kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya China katika miaka mitano ijayo, wakati huohuo pia ukitoa "orodha ya fursa" kwa dunia.
Kutimiza malengo ya kupunguza umaskini ya Ajenda ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa 2030 mapema kabla ya muda uliopangwa, kudumisha wastani wa pato la taifa kwa kila mtu unaozidi dola za Kimarekani 13,000 kwa miaka mitatu mfululizo, kujenga mfumo mkubwa zaidi duniani wa elimu, uhakikishaji wa jamii na afya… Ujenzi wa mambo ya kisasa wenye umaalumu wa China unafuata mbinu ya kutilia maanani zaidi watu, ukihakikisha kwamba hakuna mtu yeyote anayeachwa nyuma, na unatoa mfano hai wa kuigwa kwa dunia.
Katibu Mkuu Xi Jinping alisema: "Kutimiza mambo ya kisasa ni haki isiyoweza kunyang'anywa ya nchi zote duniani", na "Matarajio ya watu katika nchi mbalimbali duniani kwa maisha bora ndiyo tunayojitahidi kuyatimiza."
Kwa kuongozwa na maono ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja, China siku zote inaunganisha maslahi ya watu wa China kwa karibu na yale ya watu wa nchi zingine, ikisukuma mbele michakato ya maendeleo ya mambo ya kisasa ya nchi mbalimbali duniani kupitia ujenzi wake wa mambo ya kisasa.
— China na Afrika zinashirikiana kusukuma mbele ujenzi wa mambo ya kisasa ulio wa haki na usawa, wenye kufungua mlango na wa kunufaishana, wenye kutilia maanani zaidi watu, shirikishi na jumuishi, rafiki kwa ikolojia, na ulio wa amani na salama. Kuanzia Mei Mosi mwaka huu, China imetekeleza sera ya kutoza ushuru-sifuri kwa nchi 53 za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia nayo, ikipanua zaidi ufikiaji wa soko la China kwa bidhaa kutoka Afrika kupitia hatua kama vile kuboresha "njia ya kijani". Hatua za ushirikiano – kuanzia ustawi wa biashara, ushirikiano wa minyororo ya viwanda, na muunganisho wa miundombinu —zinaimarisha uwezo wa Afrika kwa ajili ya kujitegemea kimaendeleo.
— China na nchi za Asia ya Kati zinafanya kazi pamoja kwa kuheshimiana, kuaminiana, kunufaishana na kuungana mkono, zikisukuma mbele ujenzi wa pamoja wa mambo ya kisasa kupitia maendeleo yenye sifa bora. Miradi kama vile Reli ya China–Kyrgyzstan–Uzbekistan, Barabara Kuu ya China–Tajikistan, Eneo Maalum la Kielelezo la Sayansi ya Teknolojia ya Kilimo cha Kisasa la China–Uzbekistan, na Karakana za Luban imevishinda vizuizi vya kijografia na kiufundi, ikifungua uwezekano mkubwa kwa maendeleo ya mambo ya kisasa ya kikanda.
— China na nchi za Latini Amerika zimekuwa zikishiriki katika kubadilishana kwa kina uzoefu wa utawala, kutekeleza miradi kadhaa "midogo lakini yenye kupendeza" ya kuboresha maisha ya wananchi, kupanua ushirikiano katika nyanja zinazoibuka, na kujenga msingi imara kwa maendeleo ya pamoja kupitia hatua kama vile kutoa ufadhili wa masomo wa serikali, na kutoa mafunzo kwa wataalamu katika mbinu za kupunguza umaskini.
— Kuanzisha "Mfumo wa Ushirikiano wa Vipengele-Vitano" na nchi za Kiarabu, kujenga "Majukwaa Makubwa Sita ya Ushirikiano" na nchi za visiwa vya Pasifiki, kutoa fursa ya ushuru-sifuri kwa asilimia 100 ya bidhaa zinazostahiki kwa nchi zote zilizo nyuma kimaendeleo ambazo zina uhusiano wa kidiplomasia na China… Katika njia ya kufuata kwa pamoja ndoto ya mambo ya kisasa, "Watu wa China si tu wana matumaini kwa maisha mazuri wenyewe, bali pia wanawatakia maisha mazuri watu wa mataifa yote mengine.”
Katibu Mkuu Xi Jinping ametoa mapendekezo manne ya kimataifa, yakitoa mwelekezo kwa ajili ya kuhimiza ujenzi wa mambo ya kisasa duniani wenye sifa ya maendeleo ya amani, ushirikiano wa kunufaishana na ustawi wa pamoja.
Pendekezo la Maendeleo Duniani linajenga maafikiano ya pamoja juu ya kuhimiza maendeleo duniani, na kuleta vichocheo vipya vya ukuaji duniani; Pendekezo la Usalama Duniani linaweka mkazo katika kutatua migogoro ya kimataifa kupitia mazungumzo na mashauriano, likijenga mazingira tulivu kwa maendeleo; Pendekezo la Ustaarabu Duniani limedhamiria kuhimiza ujumuishaji na kufunzana miongoni mwa ustaarabu, likiongeza machaguo ya njia za kuelekea mambo ya kisasa; Pendekezo la Usimamizi Duniani linalenga kuufanyia mageuzi na kuuboresha usimamizi duniani, likiwezesha watu kutoka nchi zote kuwa na hisia kubwa zaidi za kupata manufaa, furaha na usalama.
Mwezi Mei 2026, China, pamoja na nchi 53 na mashirika 9 ya kimataifa walianzisha kwa pamoja Muungano wa Washirika Duniani Kwa ajili ya Kupunguza Umaskini na Kuleta Maendeleo, wakijitolea kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja isiyo na umaskini na yenye sifa ya maendeleo ya pamoja, na hivyo kuingiza nguvu mpya katika kuharakisha mchakato wa kupunguza umaskini duniani.
Vijito vidogo vinavyotiririka hukutana kwenye bahari pana, na miale ya nyota ndogondogo huangaza njia nyeupe angani. Mapendekezo ya China yanakita mizizi kote duniani, na simulizi hai za ujenzi wa mambo ya kisasa, moja baada ya nyingine, kwa pamoja zinachora picha nzuri ya mambo ya kisasa duniani.
“Wakati wote, tunapaswa kuipa kipaumbele mioyo ya watu na maslahi ya dunia, na kufanya juhudi bila kuchoka kuongeza ustawi wa watu.”
China itaendelea kushirikiana na nchi nyingine katika njia ya kuelekea mambo ya kisasa, ikiruhusu jitihada za ujenzi wa mambo ya kisasa zenye sifa tofauti kukutana pamoja kuwa mkondo wenye nguvu kubwa wa nyakati ambao unasukuma ustawi na maendeleo duniani.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



