Milipuko kadhaa yasikika Kusini mwa Iran huku Marekani ikithibitisha raundi mpya ya mashambulizi

(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 09, 2026

TEHRAN - Milipuko kadhaa ilisikika jana Jumatano usiku katika jimbo la Hormozgan kusini mwa Iran huku makao makuu ya amrijeshi ya Jeshi la Marekani ikisema vikosi vyake vimefanya mashambulizi dhidi ya Iran kwa siku ya pili mfululizo.

Vyombo vya habari vya Iran vimesema, milipuko hiyo imesikika katika wilaya za Bandar Abbas, Qeshm, Sirik na Kisiwa cha Abu Musa cha Iran.

Shirika la habari la IRIB la kiserikali la Iran limeripoti kwamba milipuko mitatu pia ilisikika katika wilaya ya Chabahar ya kusini mashariki, na kuifanya idadi ya jumla ya milipuko huko Bandar Abbas kufikia nane, ambapo mfumo wa ulinzi wa anga wa huko ulianza kufanya kazi.

Makao makuu ya amrijeshi ya Jeshi la Marekani imesema katika taarifa yake kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba vikosi vyake "vimeanza kufanya mashambulizi ya nyongeza dhidi ya Iran ili kupunguza zaidi uwezo wao wa kutishia uhuru wa usafirishaji katika Mlango-Bahari wa Hormuz."

(Wahariri wa tovuti:Liu Mengxue,Zhao Jian)

Picha