Lugha Nyingine
IMF yapunguza makadirio ya ukuaji wa uchumi duniani mwaka 2026 kutokana na hatari za Mashariki ya Kati

Picha iliyopigwa Julai 8, 2026 ikionyesha Makao Makuu ya Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Washington, D.C., Marekani. (Xinhua/Li Rui)
NEW YORK - Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) limekadiria jana Jumatano kwamba ukuaji wa uchumi duniani utapungua hadi asilimia 3.0 mwaka 2026 kabla ya kurejea hadi asilimia 3.4 mwaka 2027.
“Hii ni chini kutoka wastani wa asilimia 3.5 ya ukuaji mwaka 2025, na pia ni chini kidogo kutoka makadirio ya asilimia 3.1 katika ripoti ya Mtazamo wa Uchumi wa Dunia ya Aprili 2026. Kupungua huko kwa kiasi kidogo kunaakisi athari za vita katika Mashariki ya Kati, ambazo kwa kiasi fulani zimefidiwa na mwenendo wa kasi inayochochewa mahitaji katika mzunguko wa teknolojia duniani, ukiendeshwa na upigaji hatua katika AI na matumizi yake,” ripoti ya Julai ya shirika hilo imesema.
Imeongeza kuwa kiasi cha biashara duniani kinatarajiwa kupungua kwa kasi kutoka asilimia 5.0 mwaka 2025 hadi asilimia 3.5 mwaka 2026 kabla ya kurejea hadi asilimia 4.3 mwaka 2027.
China inatarajiwa kukua kwa asilimia 4.6 mwaka 2026, point za asilimia 0.2 juu kuliko makadirio ya Aprili -- mojawapo ya nchi chache zenye uchumi mkubwa zilizopata marekebisho ya kwenda juu.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



