Lugha Nyingine
Kampuni za China zachunguza fursa kwenye Wiki ya Uwekezaji na Biashara ya Ghana

Mwonyeshaji bidhaa wa China (kushoto) akimwelezea mtembeleaji vifaa vyake kwenye Wiki ya Uwekezaji na Biashara ya Ghana na Maonyesho ya Ujenzi ya Afrika ya siku tatu, Accra, Ghana, Julai 8, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)
Shughuli ya mkutano na maonyesho iliyounganisha Wiki ya Uwekezaji na Biashara ya Ghana (GITW), Maonyesho ya Ujenzi ya Afrika na Megawati Afrika ililenga kuchochea uwekezaji katika biashara, ujenzi, miundombinu na nishati, wakati huohuo kusisitiza uwekezaji wa moja kwa moja wa kigeni, maendeleo ya miji ya kisasa, nishati mbadala, usafiri wa vyombo vya umeme na uvumbuzi wa ngazi ya chini wa kampuni changu nchini Ghana.
Shughuli hiyo ambayo imemalizika jana Alhamisi, imevutia waonyeshaji wasiopungua 100 kutoka kote duniani, miongoni mwao kadhaa wametoka China, wakitafuta kupanua uwepo wao duniani kupitia fursa za soko na ushirikiano nchini Ghana, kitovu cha Afrika Magharibi.
Xue Jun, naibu meneja mkuu wa Kundi la Duowei Union, amesema kampuni hiyo inalenga kuongeza uwepo wake kwa kutoa huduma za usanifu, utengenezaji na ufungaji wa vifaa kwa kampuni zinazojihusisha na biashara za maghala na karakana nchini Ghana na Afrika Magharibi.
Mwonyeshaji bidhaa mwingine wa China ni Kundi la China Lesso Holdings, mtengenezaji wa mabomba ya ujenzi na makazi, vifaa vya samani za nyumbani, paneli za jua, inveta na mifumo ya kuhifadhi nishati. Mai Jiaqi, mwakilishi wa mauzo wa kundi hilo, amesema kampuni hiyo inaona fursa kubwa nchini Ghana kutokana na sekta ya nyumba inayoshamiri, ikiwa na majengo makubwa ya makazi na ya kibiashara, vilevile hoteli na miundombinu mingine ya sekta ya ukarimu, inayoibuka.

Mtembeleaji akiwa ameketi ndani ya gari linalotumia umeme kwenye Wiki ya Uwekezaji na Biashara ya Ghana ya siku tatu na Maonyesho ya Ujenzi ya Afrika, Accra, Ghana, Julai 8, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Watembeleaji wakitazama gari linalotumia umeme kwenye Wiki ya Uwekezaji na Biashara ya Ghana ya siku tatu na Maonyesho ya Ujenzi ya Afrika, Accra, Ghana, Julai 8, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)

Watembeleaji wakiwa wamepanda pikipiki inayotumia umeme kwenye Wiki ya Uwekezaji na Biashara ya Ghana ya siku tatu na Maonyesho ya Ujenzi ya Afrika, Accra, Ghana, Julai 8, 2026. (Picha na Seth/Xinhua)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



