Lugha Nyingine
Xi Jinping kuhudhuria kwenye ufunguzi wa Mkutano wa AI Duniani 2026 na kutoa hotuba kuu
BEIJING - Mkutano wa AI Duniani 2026 na Mkutano wa Ngazi ya Juu kuhusu Usimamizi wa AI Duniani vitafanyika Shanghai kuanzia Tarehe 17 hadi 20 mwezi huu. Rais wa China Xi Jinping atahudhuria kwenye ufunguzi wa mkutano huo na kutoa hotuba kuu, Lin Jian, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China ametangaza jana Jumatatu.
Akijibu swali husika, msemaji huyo amesema Rais Xi atafafanua kuhusu sera, msimamo, maono na mapendekezo ya China juu ya maendeleo na usimamizi wa AI kwenye ufunguzi wa mkutano huo wenye kaulimbiu ya "Washirika wa AI, Kujenga Pamoja Mustakabali."
Lin ameongeza kuwa China imewaalika maofisa wa serikali na watu wa sekta mbalimbali, vyuo vikuu na taasisi za utafiti kutoka nchi mbalimbali duniani, pamoja na wakuu wa mashirika ya kimataifa kufurahia pamoja wakati huo nchini China.
Msemaji huyo akisema uvumbuzi wa kiteknolojia wa AI unapitia mafanikio mapana na kuonyesha nguvu hai ambayo haijapata kuonekana, na maendeleo ya namna hiyo yameleta fursa na changamoto kwa jumuiya ya kimataifa, na kufanya usimamizi wa AI kuwa mada muhimu ya zama tulizo nazo.
"Katika miaka ya hivi karibuni, kwenye nyanja ya AI, China siku zote inatekeleza mapendekezo manne ya Dunia, na Pendekezo la Usimamizi wa AI Duniani yaliyotolewa na Rais Xi," amesema Lin, akidhihirisha kuwa China imejitolea kutoa bidhaa za umma za kimataifa, kufanya vitendo halisi kwa kutetea matumizi ya AI yalete ustawi kwa wote, na kusaidia Nchi za Dunia ya Kusini kuimarisha ujengaji wa uwezo, juhudi hizo zote zinapongezwa sana na jumuiya ya kimataifa.
"Kwa kupitia mkutano huu, China inatarajia kujenga jukwaa kwa pande mbalimbali kuongeza hali ya kuaminiana, kukusanya maoni ya pamoja, na kuzidisha ushirikiano ili kuhimiza maendeleo mazuri, salama na yenye utaratibu ya AI, na kuufanya mkutano huu kuwa mnara katika historia ya maendeleo ya AI," Lin amesema.
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



