Lugha Nyingine
Iran yasema itaacha kutekeleza wajibu kama Marekani itaendelea kukiuka majukumu ya MoU

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wa wiki mjini Tehran, Iran, Julai 13, 2026. (Xinhua/Shadati)
TEHRAN - Iran itaacha kutimiza wajibu wake kama Marekani itaendelea kukiuka majukumu chini ya nyaraka ya makubaliano ya pande mbili ya mwezi uliopita (MoU), msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei amesema jana Jumatatu.
MoU bila shaka imeingia katika "kipindi cha mgogoro," huku Iran haijawahi kamwe kuwa upande uliokiuka ahadi chini ya makubaliano hayo kwanza,” Baghaei amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari wa wiki katika mji mkuu Tehran.
Ameishutumu Marekani kwa kuendelea kukiuka wajibu wake na kuharibu vifungu na vipengele vya MoU katika kipindi cha wiki zilizopita.
Iran inashikilia kanuni ya "wajibu kwa wajibu" katika kutekeleza vifungu vya MoU hiyo. Pale upande mwingine unapoendelea kutimiza wajibu wake, "sisi pia tutatekeleza ahadi zetu," amesema.
Alipoulizwa kama diplomasia inabaki wazi kufuatia hali mpya ya hivi punde inayoendelea, Baghaei amesema diplomasia, kama chombo na nyenzo, kamwe haikomi.
"Kila inapobidi, Iran hutumia njia na mbinu zote kutetea maslahi na usalama wa taifa," ameongeza.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Esmaeil Baghaei akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari wa wiki mjini Tehran, Iran, Julai 13, 2026. (Xinhua/Shadati)
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma



