Lugha Nyingine
Reli ya SGR ya Kenya yashuhudia ongezeko la mizigo baada ya kuanza kwa sera ya ushuru-sifuri ya China
(Tovuti ya Gazeti la Umma) Julai 14, 2026
![]() |
| Picha hii iliyopigwa Julai 10, 2026 ikionyesha treni ya mizigo kwenye Reli ya SGR ya Mombasa-Nairobi ikiingia katika Stesheni ya Reli ya Port Reitz, Mombasa, Kenya. (Xinhua/Xie Jianfei) |
Tokea Mei 1, China ilianza kutekeleza sera ya ushuru-sifuri kwa bidhaa kutoka nchi 53 za Afrika ambazo inadumisha uhusiano wa kidiplomasia nazo.
Kwa mujibu wa Kampuni ya Uendeshaji wa Reli ya Africa Star, Reli ya SGR ya Kenya iliendesha treni za mizigo jumla ya 3,931 katika nusu ya kwanza ya mwaka 2026, ikisafirisha tani milioni 4.278 za mizigo, huku wastani wa kiwango cha mizigo wa kila siku ukiongezeka kwa asilimia 12.3 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
Usafirishaji wa makontena kutoka Nairobi hadi Mombasa uliongezeka kwa kasi mwezi Mei na Juni kufuatia utekelezaji wa sera ya ushuru-sifuri, ambao ni sawa na ongezeko la asilimia takriban 44 ikilinganishwa na wastani wa kila mwezi uliorekodiwa mapema mwaka huu.
(Wahariri wa tovuti:Song Ge,Zhao Jian)
Kuhusu Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma
people.cn © Tovuti ya Gazeti la Umma




